Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Saturday, June 20, 2015

NI WADHAMINI 1905 WAJITOKEZA KUMDHAMINI MH. MEMBE MTIA NIA KATIKA UGOMBEA NAFASI YA URAIS KWA TIKETI YA CCM- MKOA WA SINGIDA


Na,  Doris Meghji Jumamosi Juni 20,2015
Singida


Mh. Bernard Membe akihutubia wakazi na wananchi wa manispaa ya singida baada ya kudhaminiwa na wanaccm 1905 katika mchakato wa kutafuta wadhamini wa kumdhanini nafasi hio ya rais(Picha na Doris Meghji)
Jumla  ya wanachama 1905  wa CCM wamejitokeza kumdhamini mgombea wa nafasi ya Urais Mh.Bernard Membe  mkoani Singida ambapo katika kutoa shukurani zake za dhati mgombea huyo amesema  siku akipata kuwa rais wa jamuhri ya Muungano wa Tanzania kupitia  chama hicho atataka akumbukwe kwa kuleta utawala bora ulio wakweli na unaondoa dhuluma, unaoleta adilifu,unazozingatia miiko ya uongozi na mengine mengi ikiwa ni pamoja na kutoa adhabu watoa rushwa na mafisadi nchini.

Mh. Bernard Membe akihutubia wakazi na wananchi wa manispaa ya singida baada ya kudhaminiwa na wanaccm 1905 katika mchakato wa kutafuta wadhamini wa kumdhanini nafasi hio ya urais(Picha na Doris Meghji)
Mh. Bernard Membe ameweka hayo  adharani juzi wakati akitafuta wadhani wa kumdhani katika kugombea kinyang’anyiro hicho cha nafasi ya urais kwenye viwanja  vya ofisi ya CCM mkoa wa Singida


Mh. Bernard Membe akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CCM wilaya singida wakati akiwasili katika viwanja ya ofisi ya CCM mkoa wa Singida (Picha Doris Meghji)
 Membe amesema katika suala ilo la utawala bora atahakiisha anarekebisha vipengele vya sheria vinavyowalinda wala rushwa na mafisadi nchini hasa katika kipengele cha anayetoa na kupokea rushwa wate wakawa wakosaji.
Mh. Membe akinong’ona jambo na mmoja ya watu watu waliojitokeza kudhamnini mtia nia huyo(Picha na Doris Meghji)
Aidha katika kutafuta wadhamini hao mtia nia Membe amesema lengo la kutia nia hiyo katika kinyang’anyiro hicho amejiona  sifa za kugombea nafasi hiyo anazo na anafaa kuwa rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kupitia CCM.

Magdalena Ndwete katibu wa CCM wilaya Singida mjini akisoma idadi ya wanachama wa CCM waliojitokeza kudhamini mtia nia Membe mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji)

Vijana wa boda baoda akiongoza msafara wa mtia nia Membe wakati akiwasili katika ofisi za CCM mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji)

Mh. Bernard Membe mtia nia wa nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM akisubiri kupanda jukwahani kwa ajili ya kutoa shukrani kwa waliojitokeza kudhamini mkoa wa Singida (Picha Doris Meghji)

Wananchi na wakazi wa manispaa ya Singida wakimsubiri Mtia nia ya kugombea nafasi ya urais Mh. Bernard Membe waziri wa Wizara ya mambo ya nchi na ushirikiano wa Kimataifa (Picha na Doris Meghji)

Mh. Bernard Membe akiongozana na viongozi na wadhamini waliojitokeza kudhamini mtia nia huyo katika ofisi ya CCM mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji)
Hata hivyo kwa mujibu wa Mangula, mgombea wa CCM atakaeteuliwa kukiwakilisha chama hicho katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25 atakuwa na sifa hizi :
1. Awe na uwezo mkubwa wa kuliongoza taifa kwa kuzingatia uzoefu wake katika uongozi wa shughuli za serikali, umma na taasisi.
2. Awe mwadilifu, mwenye hekima na busara.
3. Awe na angalau elimu ya chuo kikuu au inayolingana na hiyo.
4. Awe ni mtu mwenye upeo mkubwa wa kuweza kudumisha muungano, amani, umoja na mshikamano wa kitaifa uliopo.
5. Awe mwepesi wa kuona mbali na asiyeyumbishwa, mwenye uwezo wa kufanya maamuzi ya busara kuhusu masuala nyeti ya kitaifa kwa wakati unaofaa.
6. Awe na upeo mkubwa na uwezo usiotiliwa shaka kuhusu masuala ya kimataifa na anayeweza kuwa kiongozi imara atakayetuunganisha na mataifa mengine.
7. Asiwe mtu mwenye hulka ya kidikteta au fashisti, bali awe mtu anayeheshimu katiba, sheria, utawala bora na kanuni zilizopo.
8. Awe ni mtu anayeweza kutetea wanyonge na haki za binadamu.
9. Awe mzingatiaji makini na asiye mtu anayejitafutia umaarufu binafsi.
10. Awe mtu wa mstari wa mbele kuzitekeleza sera na ilani ya CCM na awe ni mpenda haki na jasiri wa kutetea maslahi ya umma, kupambana na dhuluma na uonevu.
11. Mtu asiyetumia nafasi yake ya uongozi kujilimbikizia mali.
12. Awe ni mtu anayekubalika na wananchi
13. Awe ni mtu makini katika kuzingatia masuala ya uwajibikaji.

Mwisho.

Tuesday, June 16, 2015

MATUKIO KATIKA PICHA - KATIKA ZOEZI LA KUMDHAMINI MH. EDWARD LOWASSA MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CCM LEO

PICHA NA DORIS MEGHJI 
Baadhi ya wadhamini wanachama wa CCM wakiendelea kusaini katika fomu ya udhamini kwa ajili ya kumdhamini Mgombea Edward Lowassa (Picha na Doris Meghji)

Hivi ndivyo wananchi na wanachama wa CCM walivyojitokeza leo kudhamini Mgombea urais Mh. Edwaerd  Lowassa leo katika viwanja vya CCM mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji)


Wana CCM wakimsubiri Mh. Edward Lowassa kwa ajili ya kumdhamini mgombea huyo  mkoani Singida leo katika viwanja vya CCM mkoa wa Singida( Picha na Doris Meghji)

baadhi ya wanachama wanawake wa ccm waliofika katika zoezi la kumdhamini Mh. Mgombea Urasi Edward Lowassa (Picha na Doris Meghji)
Baadhi ya wazee wakimsubiri Mgombea wa nafasi ya urais leo Mh. Edward Lowassa katika viwanja va CCM mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji)

Mh. Edward Ngoyai Lowassa akiwasalimia  leo wananchi waliofika kumlaki katika zoezi la kutafuta wadhamni wa CCM  kwenye ugombea urais kwa tiketi ya CCM.( Picha na Doris Meghji)
Mh. Edward Lowassa akisalimia wananchi n na viongozi wa wanachama wa CCM mkoa wa Singida leo katika ofisi za CCM mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji)
Bi Sarah Nalingigwa mmoja wa wanachama  wa CCM mkoa wa Singida akimsumbili mgombea urais kwa Tiketi CCM Mh. Edward Lowassa kwenye zoezi la udhamnini leo katika viwanja vya CCM mkoa wa Singida (picha na Doris Meghji)


WANANCHI WA MKOA WA SINGIDA WAJITOKEZA KWA WINGI LEO KUMDHAMINI _ MH. EDWARD LOWASSA KATIKA NAFASI YA UGOMBEA URAIS

Na, Doris Meghji  Jumanne Juni 16,2015
Singida
Mgombea Urais wa CCM Mh. Edward Lowassa akihutubia wananchi na wakazi wa mkoa wa Singida katika ofisi za chama hicho leo katika zoezi la kutafuta wadhamini wa kudhamini kugombea nafasi hiyo ndani ya chama hicho (Picha na Doris Meghji)

Zaidi ya wanachama 22,elfu  wa CCM wamejitokeza  leo kumdhamini  Mgombea  wa nafasi ya urais wa Chama hicho MH. Edward  Lowassa  mkoani Singida
Mh. Edward Lowassa akipanda jukwaani tayari kwa kuhutubia umati wa wananchi na wanachama wa mkoa wa singida waliojitokeza kumdhamini leo katika kinyang’aniro hicho.(Picha na Doris Meghji)

Katika ziara hiyo mkoani hapa Mgombea nafasi hiyo ya urais  Mh. Edward Lowassa amewashukru wananchi na viongozi wa CCM  mkoa wa Singida kwa kujikitokeza kwa wingi na kuonyesha kuwa na imani kubwa kwake kwa kumdhamini kwa idadi hiyo ya wanachama wa chama hicho.
Baadhi ya wananchi walijitokeza leo kumsikiliza na kudhamini Mh. Edward Lowassa leo katika kinyang’anyiro cha  kugombea nafasi ya urais ndani ya CCM (Picha na Doris Meghji)

Mgombea huyo amezieleza sababu zake za kugombea nafasi hiyo kwa lengo  kubwa la  kuwaongoza watanzania kutoka katika wimbi la umaskini licha ya utajiri wa rasilimali zilizopo katika nchi hii.
Mh. Edward Lowassa akieleza sababu za yeye kugombea nafasi hiyo ya urais ndani ya CCM kwa wakazi wa mkoa wa singida leo katika viwanja vya CCM mkoa.(picha Doris Meghji)

Mh. Lowassa anasema “Nagombea nafasi hii kwa kwababu nimechukizwa na kuchoshwa na umaskini katika nchi yetu, toka 1962 baba wa taifa alisema tuna maadui  wakubwa watatu maradhi,ujinga na umaskini leo umaskini umekithiri  kana kwamba hatuko kwenye nchi yenye rutuba na yenye rasilimali nyingi  sana  za utajiri kiasi hiki na wananchi wake kuendelea kuwa  maskini  mi nakataa kabisa” alisisitiza Mgombea  Lowassa.

Wananchi wakimsikiliza mh. Edward Lowassa leo katika viwanja vya CCM mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji)

Aidha amesema Mwenyezi  Mungu akibari  na kupata ridhaa wa jambo hilo ataendesha nchi mchaka mchaka atafanya hivyo katika elimu kilimo, ajira kwa vijana na maeneo mengine kwa rasilimali nyingi  zilizopo katika nchi hii.
Wananchi wakimsikiliza mh. Edward Lowassa leo katika viwanja vya CCM mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji)
Hata hivyo amewataka wajiandikishe kwa wingi katika daftari la kudumu la wapiga kura ili iwape fursa ya kumchagua kiongozi huyo Oktoba 25 mwaka huu.


Mh. Edward Lowassa akihutubia wananchi wa mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji)
Mh. Edward Lowassa akiwa ni mgombea wa 15 kufika katika mkoa wa singida kutafuta wadhamini watakao mdhamini kwa nafasi hiyo kwa chama cha mapinduzi ambapo wilaya Singida mjini wadhamini 5272,Iramba 4201,Singida vijijini 4018,Ikungi 3122,Manyoni wadhamini 3920 huku wilaya ya Mkalama wadhamini 2225 wamejitokeza kumdhamini Mgombea huyo.

Viongozi wakimpokea Mh. Edward Lowassa katika zoezi hilo la kutafuta wadhamini (picha na Doris Meghji)
Wajumbe wa NEC mkoa wa Singida na Simiyu wakisalimia wananchi pamoja na mbunge viti Maalum mkoa wa Singida Diana Chilolo leo katika zoezi la kumdhamini mgombea urais kwa tiketi ya CCM ( Picha na Doris Meghji)
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Singida Vijijini Narumba Hanje akiwasalimia wananchi waliojitokeza kumsikiliza Mgombea Edward Lowassa.(Picha na Doris Meghji)
Magdalena Ndwete katibu wa CCM wilaya Singida mjini akitoa taarifa ya idadi ya wadhamini waliojitokeza kudhamini mgombea huyo (Picha na Doris Meghji)
Mgana Msindai Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida akimkaribisha mh. Edward Lowassa kuongea na wananchi wa mkoa wa Singida leo katika viwanja vya ofisi ya CCM mkoa.(Picha na Doris Meghji)
Mwisho.






Monday, June 15, 2015

WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA KUPIGA KURA -

Na, Doris Meghji  Jumapili Juni 14,2015
Singida- Manispaa

Joseph Mchina Mkurugenzi wa manispaa ya Singida akitembelea  leo kituo cha kuandikisha wapiga kura mtaa wa Utemini (Picha na Doris Meghji)

Zoezi la uandiishaji wa  wananchi katika daftari la kudumu la kupiga kura awamu ya mwisho ndani ya manispaa ya Singida imeanza leo ikizihusisha jumla ya kata nne za manispaa hiyo
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura leo kituo cha mtaa wa utemini shule ya msingi utemini (Picha na Doris Meghji)


Katika zoezi hilo leo  yametolewa maelekezo  kwa waandikishaji wa vituo vya  hivyo kuhakikisha wanawaandikisha wananchi wa mtaa husika na si vinginevyo ikiwa ni pamoja na vijana ambao wenye  umri mdogo kuhitaji vithibitisho vya vyeti vyao vya kuzaliwa au kupata barua toka kwa mwalimu mkuu alipomalizia darasa la saba lengo likiwa kudhibiti mamluki katika zoezi hilo.
Mohamed Kipamila mmoja wa waandikishaji katika kituo cha mtaa wa saba saba akimhoji kijana wakati wa zoezi hilo leo katika shule ya msingi saba saba.(Picha na Doris Meghji)

Akitoa maelekezo hayo msimamizi mkuu wa zoezi la uandikishaji wa wananchi katika daftari la kudumu la kupiga kura na  mkurugenzi wa manispaa ya Singida Joseph Mchina anasema  “ninamelekezo aina mbili wale wananotakiwa kujiandikisha katika kituo hii ni wale wanaishi mtaa wa utemini na sio nje ya mtaa wa  utemini. kila mtaa nimepeleka mashine hivyo hakuna haja mtu wa saba saba kuja kujiandikishia hapa utemini,la pili wale vijana wenye umri mdogo nihahtaji uthibitisho wa umri wao.
Wananchi na wakazi wa mtaa wa Stesheni walivyojitokeza leo katika kituo cha SIDO kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura (Picha na Doris Meghji)

Ninahitaji cheti cha kuzaliwa,au barua toka kwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi alipomalizia darasa la saba au barua toka kwa mwenyekiti wake wa mtaa ndio nimruhusu kujiandikisha maana kuna vijana nawaona ni hapa ni  wadogo hawana umri huo wa miaka 18.” Asisitiza Mkurugenzi Mchina.
Zoezi la uandikishaji likiendelea katika Kituo cha Saba Saba (Picha na Doris Meghji)

Katika zoezi hilo la awamu ya mwisho ya kujiandikisha ndani ya manispaa ya Singida inahusisha kata ya Utemini, Mandewa,Mughanga na Mitunduruni  hivyo mkurugenzi wa manispaa hiyo amewataka wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika daftari hilo la kudumu
Hivi ndivyo kazi ikifanyika leo katika zoezi la uandiishaji mtaa wa Saba saba (Piha na Doris Meghji)

Hata hivyo zoezi hilo linatarajiwa kumalizika tarehe 20 mwezi huu kwa manispaa ya Singida na mkoa kwa ujumla.
Kituo cha SIDO cha uandikisha wakazi wa mtaa wa stesheni walivyojitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la kupiga kura leo majira ya saa sita adhuhuri.(Picha na Doris Meghji)

Mtendaji wa mtaa wa sabasaba Anneth Mayengela akiita majina ya watu wanaotakiwa kuandiishwa kwa muda huo(Picha na Doris Meghji)

Wakazi wa mtaa wa saba saba kata ya utemini waliofika kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura (Picha na Doris Meghji)
Vijana wakisubiri kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura (picha na Doris Meghji)

MWISHO.


Thursday, June 11, 2015

DR. MWELECELE MALECELA APATA WADHAMINI ZAIDI YA 70 MKOANI SINGIDA KATIKA KUGOMBEA NAFASI HIYO YA URAIS NDANI YA CCM

 HABARI KATIKA PICHA – DR. MWELECELE MALECELA AKIWA MKOANI SINGIDA KUTAFA WANACHAMA WA CCM KUMDHAMINI KATIKA KUGOMBEA NAFASI HIYO YA URAIS  


Dr. Mwelecela Malecela akisaini mmoja ya vitabu vya wageni katika ofisi ya CCM mkoa wa singida leo majira ya saa 4:52 asubuhi.(Picha na Doris Meghji)

Hizo ni kadi za CCM zaidi ya 70 ambazo wadhamini wamemdhamini waliojitokeza kumdhamini Mgombea nafasi ya urais Dr. Mwelecele Malecela leo mkoani Singida.(picha na Doris Meghji)


Dr. Mwelecele Malecela akisaini vitabu vya wageni leo majira ya saa 4: 52 asubuhi katika ofisi za CCM mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji)





DR. MWELECELE MALECELA MGOMBEA NAFASI YA URAIS KWA TIKETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI MWANAMKE WA KWANZA BARA KUGOMBEA NAFASI HIYO AKIWA MKOANI SINGIDA KUPATA WADHAMINI WATAKAO MDAHAMINI KWA CHAMA HICHO.

AKIWASALIMIA BAADHI YA WANACHAMA WALIOJITOKEZA
 
Bi Fatma Nkanghaa akitoa neno leo la kumtia moyo Mgembea nafasi ya urais mwana Mama DR. Mwelecele Malecela Leo aktika ofisi ya CCM mkoa wa Singida( piha na Doris Meghji)




Kushoto ni Katibu wa CCM wilaya ya Singida mjini Magdalena Ndwete,akifuatiwa na Dr. Mwelecela Malecela mgombea wa nafasi hiyo ya urais,kulia ni Margareth Malecela Katibu wa uwt wilaya ya Singida mjini na Mama Mziray Mwenyeiti wa uwt wilaya ya Singida mjini,na wakina baba waliojitokeza kudhanini Mgombea Urais hiyo leo mkoani singida(Picha na Doris Meghji)


DR. MWELE AMEWAOMBA WANACHAMA NA WADHAMINI HAO KUSHIRIKIANA NAYE KWA HALI NA MALI HASA KATIKA MCHAKATO HUO WA KUGOMBEA NAFASI HIYO YA URAIS NCHINI.

Hata hivyo  idadi ya wadhamini wanaohitajika katika kila mkoa ni wadhamini 45, zaidi ya wanachama 70  CCM wamejitokeza kudhamini mgombea huyo wa nafasi ya urasi kwa chama cha Mapinduzi mkoani  Singida ambapo zoezi hilo limefanyika  leo makao makuu ya mkoa wilaya ya  Singida mjini .
DR. Mwele akiwa ametoka jana mkoani Tabaora kutafuta wahdamini waliomdhanini kwa CCM leo mkoani Singida baada ya zoezi hilo ameelekea mkoani Manyara kudhaminiwa na mwanachama wa chama hicho.
MWISHO.



Kushoto ni katibu wa CCM wilaya Singida mjini katikati ni mtoto Alen mtoto wa mmoja wa wadhanini waliojitokeza kudhamini Mgombea Dr. Mwelecele kulia ni Mgombea nafasi ya urais DR. Mwelee leo akiwa katika ofisi ya CCM mkoa wa Singida( Picha na Doris Meghji)




Dr. Mwelecela Malecela akiwa na baadhi ya wahdanini waliojitokeza kumdhanini katika nafasi hiyo ya Urais  leo ofisi za CCM mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji)



 Dr. Mwelecele Malecela Mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM akimkumbatia Bi Fatma Nkanghaa mara baada ya kutoa neno mara baada ya kudhaminiwa Mgombea Dr. Mwele.(picha na Doris Meghji)


Ni Dr. Mwelecela Malecela akionyesha bagi la fomu za ugombea urais leo katika ofisi ya CCM mkoa wa Singida Mara baada ya wadhamnini hao kumdhani mgombea huyo katika nafasi hiyo ya urais (picha na Doris Meghji)




Ni Dr. Mwelecela Malecela akionyesha bagi la fomu za ugombea urais leo katika ofisi ya CCM mkoa wa Singida Mara baada ya wadhamnini hao kumdhani mgombea huyo katika nafasi hiyo ya urais (picha na Doris Meghji)

Monday, June 1, 2015

UCHAGUZI MKUU KUFANYIKA KAMA ULIVYOPANGWA - ASEMA JAJI LUBUVA



Na, Doris Meghji  Jumatatu Juni 10,2015
Singida

Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) imesema uchauguzi mkuu wa kuchagua rais, wabunge na madiwani utafanyika kama ulivyopangwa Oktoba 25 mwaka 2015.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa tume  hiyo taifa (NEC) Jaji Damian Lubuva mkoani Singida katika ziara yake ya kutembelea na kuaona   jinsi zoezi la kuandikisha wananchi katika daftari la kudumu la kupiga kura jimbo la Singida mjini.

“uchaguzi utafanyika siki hiyo ya Jumapili Oktoba 25 mwaka huu kama ulivyopangwa hii ni kutokana na wenzetu wa Zanzibar walikwisha tangaza na kukamilisha maandalizi kwa wao kufanya uchaguzi siku hiyo ya Jumapili Oktoba 25 .Hatuwezi nchi moja kufanya uchaguzi siku mbili tofauti alisistiza Jaji Lubuva”

Hii ni katika kutolea maelezo kutoka kwa baadhi ya wabunge kuhoji juu ya uchaguzi kufanyika siku hiyo ya Jumapili na sio siku nyingine katika juma ispokuwa Jumapili

Hivyo amesema Tume ya uchaguzi imeliona hilo na kuahidi kulifanyia kazi katika chaguzi zingine zijazo kwa kupanga siku za uchauguzi kufanyika siku nyingine na sio siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kwa kuwa ni siku ambazo wananchi wa Tanzania  wanakwenda katika nyumba zao za ibada.
Hapo aliendelea kuwahakikishia watanzania kuwa uchaguzi wa mwaka huu utafanyika siku hiyo ya jumapili mwenyekiti huyo wa NEC.

Aidha kwa upande mwingine Mwenyekiti huyo wa NEC ameliomba jeshi la polisi nchini kuimarisha ulinzi na usalama kwa maafisa wa TUME katika vituo ikiwa ni baada ya tukio lililo wapata maafisa wa TUME hiyo wilayani Mumba mkoani Mbeya kwa kuvamiwa na watu wanaodhanini ni majabamzai na kwajeruhi maafisa hao.

Naye msimamizi wa uchaguzi jimbo la singida mjini mkurugenzi wa manispaa ya Singida Joesph Mchina  amesema zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linaendela vizuri kwa kuwa awamu ya kwanza wamefanikiwa kuandikisha wananchi kwa wastani wa asilimia 86 katika daftari hilo liliohusisha kata nne za Mtipa Uhamaka Mwankoko na Mtamaa 

hivyo anatoa wito kwa wananchi wa maeneo ya awamu ya pili ambazo ni kata ya Minga,Mungu Maji,Unyambwa  na … kujitokeza kwa wingi kwenda kujiandikisha ikiwa ni moja ya haki yao kidemokrasia kwa kuwapa tiketi ya kuchagua viongozi watakao waongoza katika uchaguzi mkuu ujao.
Mwisho.