Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Monday, August 17, 2015

UCHAGUZI WA MWAKA HUU SIO KAMA UCHAGUZI WA MWAKA 2010 WANACCM MKOA WA SINGIDA WAASWA KUTOBWETEKA - NAOMI KAPAMBALA

Na, Doris Meghji Jumatatu Agosti 17,2015
Singida
Wanachama wa CCM mkoa na baadhi ya viongozi wakati wa sherehe za kumuaga Katibu Naomi kapambala ukumbi wa Rafiki Resort manispaa ya Singida 
Viongozi na wanachama wa chama cha Mapinduzi wameaswa kutolala kwa kuwa uchaguzi wa mwaka huu sio uchaguzi wa kawaida hivyo wametakiwa kufanya kampeni kwa hali na mali ili CCM ishinde kwenye uchaguzi mkuu huo Oktoba 25 mwaka huu.
Huyu ni Mussa Sima Mgombea wa nafasi ya ubunge jimbo la singida mjini aliyeteuliwa na chama hicho mara baada ya utata mwingi kugubigwa matokeo ya uchaguzi huo jimbo la singida mjini akiwa na Bi Yagi Kiaratu Mgombea pekee mwanamke wa nafasi ya udiwani kata ya majengo manispaa yas ingida  akiwa kwenye hafla ya kumuaga aliyekuwa katibu wa CCM mkoa wa singida na Kuhamishiwa mkoani Kigoma ( picha na Doris Meghji)
Kauli hiyo imetolewa na Naomi Kapambala katibu wa CCM mkoa wa Kigoma wakati wa sherehe za kuagwa na wanaccm mkoa wa Singida alipokuwa akifanya kazi kabla ya kuhamia mkoani Kigoma
“upinzani uliopita miaka 10 sio upinzani wa leo hivyo tusibweteke watendaji tuendelee kuwa na ushirikiano kwa kuwa uchaguzi wa miaka hii kushinda  ni kwa kijipanga na kufanya kazi bila kulala” kapambala aliwaasa wanaccm hao
Huyo ni Martha malata akisalimia na kutoa neno kwa wanachama na kumshukru Katibu Kapamabala kwa uongozi wake pindi alpokuwa mkoani Singida kwenye ukumbi wa Rafii Resort katika sherherhe ya kumuaga  iliyoandaliwa na wanachama na viongozi wa chama hicho mkoani Singida ( Picha na Doris Meghji)
Katika kusisitiza jambo hilo amewataka wabunge na madiwani viti maalum kufanyakazi na kuhakikisha ushindi kwa chama hicho kwa kuwa ushindi wa chama hicho katika majimbo na kata ndio itawapa fursa ya wao kuwa wabunge na madiwani nchini.
Wanachama wa CCM mkoa na baadhi ya viongozi wakati wa sherehe za kumuaga Katibu Naomi kapambala ukumbi wa Rafiki Resort manispaa ya Singida.

“Wale watakaofanya kazi vizuri na kuhakikisha CCM inashinda ndio watakaoteuliwa kwa nafasi hizo za udiwani na ubunge mkoani hapo”
Ni mgombea Magareth Malecela,akifuatiwa na Rehema Shilla wagombea wa viti maalum kushoto na mgombea Valelian Kimambo mgombea udiwani Kata ya Muhanga kulia ni Angela Milembe mgombea udiwani viti maalum akiwa na mgombea ubunge jimbo la Singida mjini Mussa Sima  kwenye hafla ya kumuaga katibu Naomi Kapambalaa kumbi wa Rafiki Resort manispaa ya Singida. ( Picha na Doris Meghji)
Katibu Kapambala amewataka wanachama na viongozi wa chama hicho wae macho na makundi ya urais hasa kwa kushawishiwa kupigia mbunge wa CCM, diwani wa CCM ila kwa nafasi ya urais kupigia upinzani.
Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma Bi Naomi Kapambala alikuwa akiagwa juzi katika ukumbi wa Rafiki Resort ndani ya manispaa ya Singida ( Picha na Doris Meghji)

 amewataka wasifanye hivyo kwa kuwa kauli mbiu ya chama hicho ni mafiga matatu ya kuwachagua wagombea wa nafasi ya udiwani, ubunge, na urais wote kuwa wa chama cha Mapinduzi.
Huyo ni Mary Maziku Katibu wa CCM mkoa wa Singida aliyehamia mkoani hapa kutoka makao makuu a chama cha Mapinduzi na kushika nafasi ya Mary Chatanda ambaye ni mgombea wa nafasi ya ubunge jimbo la korogwa mjini ( Picha na Doris Meghji)
Naye katibu Mary Maziku katibu wa CCM mkoa wa Singida anayekaribishwa mkoani humo ameomba ushirikiano miongoni mwa Viongozi wa ngazi zote za wilaya na mkoa ikiwa ni pamoja na wanchama wa chama hicho mkoani humo  kufanya kazi ili kuhakikisha chama cha mapinduzi kinashinda kwa kishindo na kuhakikisha hawapotezi jimbo hata moja kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu
Huyo ni Martha malata akisalimia na kutoa neno kwa wanachama na kumshukru Katibu Kapamabala kwa uongozi wake pindi alpokuwa mkoani Singida kwenye ukumbi wa Rafii Resort katika sherherhe ya kumuaga  iliyoandaliwa na wanachama na viongozi wa chama hicho mkoani Singida ( Picha na Doris Meghji)
 Hata hivyo katika hafla hiyo ya kumuaga Katibu huyo walimtangaza Mgombea Mussa Ramdhani Sima kuwa ndio mgombea aliyeteuliwa kuipeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi mkuu jimbo la Singida mjini
Huyu ni Mussa Sima Mgombea wa nafasi ya ubunge jimbo la singida mjini aliyeteuliwa na chama hicho mara baada ya utata mwingi kugubigwa matokeo ya uchaguzi huo jimboni  akiwa kwenye hafla ya kumuaga aliyekuwa katibu wa CCM mkoa wa singida na Kuhamishiwa mkoani Kigoma ( picha na Doris Meghji)
Kutangazwa kwake kumekuja mara baada ya mizengwe ya matokeo ya uchaguzi wa kura za maoni wa CCM uliofanya na katibu wa CCM wilaya ya Singida mjini  kwa kubandika matokeo hayo Agosti 02,  majira saa tatu usiku mwaka huu matokeo ambayo yalimuonyesha  mgombea Hassani Philipo Mazala akiongoza kwenye matokeo hayo hali iliyoleta sintofahamu miongoni wa mgombea Musa Sima  na wanachama wa chama hicho wilaya ya Singida mjini.
Hao ni wanachama na viongozi akiwemo Martha Mlata Mbunge mteule wa CCM viti maalum mkoa wa Singida wakiselebuka kwenya hafla ya kumuaga Naomi Kapambala aliyekuwa katibu wa CCM mkoa wa Singida na Kuhamia Mkoani Kigoma ( picha na Doris Meghji)
katibu Kapambala alikitumikia chama hicho kwa kipindi cha miaka saba toka 2007 hadi 2014 mkoani singida  ndipo alipohamishwa kwenda mkoani kigoma.
Huyo ni Margaret Malecela diwani wa viti maalum mteule kwa ccm kwa manispaa ya Singida na Mwl Lilian Mrua kada wa chama cha mapinduzi katika sherehe a kumuaga Katibu wa CCM mkoa wa Singida Bi Naomi Kapambala na kuhamia Kigoma kwenye ukumbi wa Rafiki Resort ndani ya manispaa ya Singida ( Picha na Doris Meghji)
 Mkoa wa singida unajumla ya majimbo 8 ya uchaguzi ambayo ni jimbo la  Ikungi Mashariki, Ikungi Magharibi,Manyoni Mashariki,Manyoni Magharibi ikiwa ni pamoja na Jimbo la Singida Kaskazini,jimbo la Iramba,Mkalama na Singida mjini.
Huyo ni Martha Mlata na Aisharose Matembe wabunge wateule wa Viti maalum toka mkoa wa Singida baada ya kushinda kwenye kinag'aniro cha ubunge kupitia CCM toka UWT picha na Doris Meghji)
huku wateueliwa wa ubunge viti Maalum ni Aisharose Matembe na Martha Mlata kupitia chama cha Mapinduzi toka UWT.
Mwisho.





WAUMINI JIMBO KATOLIKI LA SINGIDA WAOMBWA KUIOMBEA AMANI NCHI YAO HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

Na, Doris Meghji Jumatatu Agosti 17 2015
Singida
Padre Vicant Alute Mlezi wa chama cha Lejio Maria Jimbo katoliki la singida akihubiri kwenye misa takatifu ya kupalizwa mama Bikira maria mbinguni ( Picha na Doris Meghji)
Waumini wa kanisa katoliki jimbo la Singida wameombwa kuendelea kumuomba mama Birkia Maria ili nchi yao  ibakie katika amani hasa katika kipindi hiki cha kuelekea  uchaguzi mkuu wa Rais wabunge na madiwani utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.
 
Sanamu ya Mama Bikira Maria ya kupalizwa Binguni ( Picha na Doris Meghji)
Kuaswa kwa waumini hao kumefanyika jana  na Padre Vincent Alute mlezi wa Lejio Maria  kanisa katoliki jimbo la Singida katika maadhimisho ya Misa Takatifu ya Kupalizwa Mbinguni kwa Mama Bikira Maria katika kanisa la Moyo Mtakatifu wa Yesu.
 
Ni wanalejio Maria wa Kanisa katoliki jimbo la Singida kwenye sherehe za kupalizwa Mama bikira Maria Mbinguni ( Picha na Doris Meghji)
Padre Alute amewataka waumini hao kumshika mkono mama bikira Maria awaombee kwa Mwanae ili nchi yao ibaki katika Amani kwa kuwa wao hawakushudia vita hivyo amewataka wasijibweteke  waumini hao  wakasahau kushika mkono Mama Bikira Maria awafundishe na kuelekeza namna ya kupendana na kumpenda mwanae Yesu Kristu.
Kwaya ya Moyo Mtakatifu wa Yesu ikiimba kataika misa tafakifu ya kupalizwa mbinguni kwa mama bikira Maria jimbo katoliki la Singida ( Picha na Doris Meghjii)
Katika kulisistiza jambo hilo Mlezi Alute amewataka waumini hao kusali kweli,  kuwa makini na kuwa na msimao thabiti kama ilivyokuwa mama Bikira Maria mtu mwenye imani kwa Mungu ,wamuamini  Mungu wasije wakabweteka wakayubishwa na kusahau ukweli mama Bikira Maria alikuwa anapenda watu na majirani kwa kuwajali na kuwathamini
Kwaya ya Moyo Mtakatifu wa Yesu ikiimba kataika misa tafakifu ya kupalizwa mbinguni kwa mama bikira Maria jimbo katoliki la Singida ( Picha na Doris Meghjii)
Hivyo amewataka wasiviombe vita kwa kuwa vita havina macho kwa kuwataka waendelee kuiombea nchi yao amani katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu kwa msaada wa mama kanisa mama Bikira Maria
Ni wanalejio Maria wa Kanisa katoliki jimbo la Singida kwenye sherehe za kupalizwa Mama bikira Maria Mbinguni ( Picha na Doris Meghji)
Katika kuadhimisha sherehe hizo jumla ya wanachama wapya 117 wa chama cha Lejio Maria  wamejiunga na kufikia idadi ya wanalejio 900 jimboni Singida.
Ni wanalejio Maria  na watumikizi wa Kanisa katoliki jimbo la Singida kwenye sherehe za kupalizwa Mama bikira Maria Mbinguni ( Picha na Doris Meghji)
Ni ndugu  Remoi mwenyeikti wa lejio Maria jimbo katoliki la Singida akitoa maelezo juu ya taratibu za kuiadhimisha siku hiyo kwa wanalejio maria pamoja na waumini wa kanisa hilo( Picha na Doris Meghji)
Ni  Mama Elimna mmoja wa viogozi wa lejio maria jimbo katoliki la Singida akisoma somo la pili katika kuadhimisha misa takatifu kwenye shererehe za kupalizwa mama Bikira Maria mbinguni.( Picha na Doris Meghji)
Mwisho.

Friday, August 14, 2015

NEC KUSHUGHULIKIA MAPEMA MAJINA YA WAPIGA KURA KWENYE DAFTRI LA KUDUMU - WADAU TOKA VYAMA VYA SIASA WAIOMBA TUME HIYO JIMBO LA SINGIDA MJINI.

Na, Doris Meghji Ijumaa Agosti 14, 2015

Singida
Mgombea wa nafasi ya udiwani aliyekuwa wa CCM sasa kuhamia CHADEMA kata ya Mandewa akiongea na wanachama na viongozi wa chama hicho wilaya ya Singida mjini kwenye ukumbi wa mikutano wa Samaki singida mjini.( Picha na Doris Meghji)
Baadhi ya Viongozi wa vyama vya Siasa ndani ya manispaa ya Singida wameiomba tume ya uchaguzi wa taifa  (NEC) kuhakikisha wanalishughulikia mapema suala la majina ya wapiga kura kutokuwepo kwenye daftari hiyo kabla ya uchaguzi mkuu huo kufanyika nchini.
Hao ni baadhi ya wanachama wa CCM waliohamia CHADEMA baada ya mgombea wao wa CCM kutochaguliwa kuwa mgombea wa chama hicho kwenye ukumbi wa Samaki wakiowa na viongozi wa CHADEMA mkoa wa wilaya ya Singida mjini.( Picha na Doris Meghji)
Kwa mujibu wa katibu mwenezi wa Siasa wa chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA) wilaya ya Singida mjini Bwana Samwel Malow ameiomba na tume hiyo kuhakikisha inashughulikia tatizo hilo jimbo la singida mjini kwa kuwa idadi kubwa ya wapiga kura waliojiandikisha haipo kwenye daftari hizo.
Huyo ni Shaban Omary Kiranga mgombea wa nafasi ya udiwani kwa tiketi ya CHADEMA akipokea kadi ya uanachama wa chama hicho baada ya kurudisha kadi ya CCM mapema wiki huu.( Picha na Doris Meghji)
Kauli hiyo ameitoa mapema wiki hii katika mkutano wa chama hicho kilipokuwa kikiwapokea baadhi ya wanachama wa chama cha Mapinduzi waliohamia chama cha Demokraisa na Maendeleo wakiwa ni pamoja na aliyekuwa mgombea wa nafasi ya udiwani kata ya Mandewa Shaban Omary Kiranga  wa toka CCM kushindwa kwenye uchaguzi  wa kura za maoni uliofanyika Agosti Mosi mwaka huu na kuhamia CHADEMA.

Moja wa wanachama waliohama CCM na kuwa wanachama wa CHADEMA mara baada ya mgombea wao kutoteuliwa kuwa mgombea wa nafasi ya udiwani kata ya Mandewa kwenye ukumbi wa Samaki ( Picha na Doris Meghji)
Kwa mujibu wa katibu Mwenezi huyo amesema katika zoezi la uandikishaji wananchi kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kata ya Madewa ilifanikiwa kuandika wapiga kura 10566 huku idadi ya majina yalioko kwenye daftari hilo baada ya kuandikishwa ni 2034 tu ndio iliyoko kwenye daftari hizo katani hapo.hivyo ameiomba tume hiyo kulishugulikia mapema tatizo hilo
 Shabani Kiranga akipeana mikono na baadhi ya viongozi wa CHADEMA mara baaada ya kurudisha kadi ya CCM nakuchukua ya CHADEMA na kupea redhaa ya kugombea nafasi hio ua udiwani kwa tiketi ya CHADEMA ( Picha na Doris Meghji)
"mandewa ni waliojiandikia 10566 idadi a majina yaliopo 2034 zaidi ya 8000 hawapo kwenye daftari hii inatisha tunaiomba tume ilishughulikia suala hili"alisistiza Malow katibu mwenezi CHADEMA Singida mjini.
Hao ni baadhi ya wanachama wa CCM waliohamia CHADEMA baada ya mgombea wao wa CCM kutochaguliwa kuwa mgombea wa chama hicho kwenye ukumbi wa Samaki wakiowa na viongozi wa CHADEMA mkoa wa wilaya ya Singida mjini.( Picha na Doris Meghji)
Hata hivyo kwa upande wa kata ya Utemini ilifanikiwa kuandikisha kwenye zoezi hilo la daftari la kudumu la wapiga kura ni 5267 na idadi ya walioko kwenye daftari hilo ni 2460 huku idadi ya wapiga kura 2807 haipo kwenye daftari hilo
Moja ya daftari la kudumu la wapiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa  Rais mbunge na diwani utakao fanyika Oktoba 25 mwaka huu( Picha na Doris Meghji)
Kutokana na tatizo hilo nilifanikiwa kuongea na Mkurugenzi wa manispaa ya Singida  Joseph Mchina  juu ya suala hilo akasema ofisi yake kwa kwa kushrikiana na NEC wanalisghulikia suala hilo hivyo amewaomba wananchi wajitokeze kwenda kuhakiki majina yao kwenye mbao za matangazo kwenye ofisi za kata za manispaa hiyo jimbo la Singida mjini.
 Hizo ni baadhi ya kadi za wanachama wa CCM zilizorudishwa na wanachama wa CCM na kuchukua kadi za CHADEMA kata ya Mandewa kwenye mkutano huo wa kuwapokea wanacha wapya toka CCM kwenye ukumbi wa Samaki Kata ya Mandewa manispaa ya Singida (picha na Doris Meghji)
Katika mkutano huo zaidi ya wanachama 13 wamehamia chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA) kata ya mandewa wilaya ya Singida mjini
Mgombea wa nafasi ya udiwani aliyekuwa wa CCM sasa kuhamia CHADEMA kata ya Mandewa akiongea na wanachama na viongozi wa chama hicho wilaya ya Singida mjini kwenye ukumbi wa mikutano wa Samaki singida mjini.( Picha na Doris Meghji)

Jimbo la Singida mjini lina jumla ya kata 18 ambapo uchaguzi wa madiwani wa kata hizo wanatarajiwa kuchaguliwa kwenye uchaguzi huo mkoani Singida
MWISHO.


ZOEZI LA UCHUKUAJI FOMU ZA KUGOMBEA NAFASI ZA UBUNGE NA UDIWANI UCHAGUZI MKUU NA CHANGAMOTO LA MAJINA YA WALIOJIANDIKISHA KWENYE DAFTRI LA KUDUM LA WAPIGA KURA

Na, Doris Meghji  Ijumaa Agosti  14,2015
Singida
Bartazary Kimario akitoka kuchukua fomu ya ugombea wa nafasi ya udiwani kwenye ofisi ya mtendaji wa kata a Utemini huku akisindikizwa na baadhi ya wananchi na makada wa CCM ya jimbo la Singida mjini 9 Picha na Doris Meghji)
Zoezi la uchukuaji wa fomu za kuwania nafasi ya ubunge na udiwani kutoka vyama mbali mbali vya siasa nchini umeanza kwa wagombea wa nafasi hizo kuchukua fomu katika ofisi za watendaji  wa kata na manispaa ya Singida mara baada ya kuteuliwa na vyama vyao kupeperusha bendera za vyama hivyo vya siasa kwenye  uchaguzi mkuu  utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Hii ni moja ya fomu za uteuzi wa ugombea udiwani toka tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) ambao mgombea anatakiwa kuijaza na kuirudisha ndani ya siku 21 zoezi ambalo limeanza rasmi Agosti 08 mwaka huu na kukamilishwa Agosti 21  kabla ya saa 10 kamili jioni kwenye ofisi hizo za watendaji wa kata jimbo la singida mjini.( Picha na Doris Meghji)
Katika zoezi hilo ambalo kwa mujibu wa ratiba ya Tume ya taifa ya uchaguzi  (NEC) zoezi hilo la uchukuaji wa fomu hizo za kugombea nafasi za ubunge na udiwani zimeanza rasmi Agosti nane mwaka huu,huku manispaa ya Singida katika kata ya Utemini mgombea wa nafasi ya udiwani kupitia chama cha Mapinduzi Bartazary Lessio Kimario amechukua rasmi  fomu ya kugombea nafasi hiyo kwa kata ya utemini
Baadhi ya wananchi walijitokeza kumsindikiza mgombea wa CCM  wa nafasi ya udiwani Bartazary Kimario wakati akienda kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo kwa kata ya Utemeni jimbo la Singida mjini ( Picha na Doris Meghji)
Mgombea huo mara baada ya kuchukua fomu hiyo ya kuwania kinyang’anyiro hicho amewaahidi wanachama na wananchi wa kata hiyo kumuunga mkono kwa kumdhanini na kumchagua kwenye nafasi hiyo ya udiwani kwenye uchaguzi mkuu kwa kuhakikishia utekelezaji wa ilani ya CCM kutekelezwa vizuri katika sekta mbali mbali hasa ya miundombinu elimu, maji na maendeleo ya jamii.
 
Baadhi ya wanachi wa kata ya utemini wakiwa kweny moja ya mikutano ya kampeni za kura za maoni ndani ya CCM katika tawi la Stesheni (Picha na Doris Meghji)

Katika suala la miundombinu Mgombea Kimario amewahadi wananchi hao kuwa barabara za kata hiyo zitatekelezwa hasa kupitia mradi wa banki ya dunia kwa kata hiyo ujenzi wa barabara mbili zitajengwa ndani ya mradi huo wa banki ya dunia kwa manispaa ya Singida
Baadhi ya wananchi walijitokeza kumsindikiza mgombea wa CCM  wa nafasi ya udiwani Bartazary Kimario wakati akienda kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo kwa kata ya Utemeni jimbo la Singida mjini ( Picha na Doris Meghji)
kwa mujibu wa mratibu msaidizi  wa uchaguzi kata ya utemii Afisa mtendaji wa kata ya utemini Bi Eva  Simon Mbelwa amesema utaratibu wa uchukuaji wa fomu za wagombea  baada ya uteuzi kwenye vyama vyao  ambazo ni fomu ya ugombea na fomu ya maadili ambazo kila mgombea anachukua nakala nne.
Bi  Eva Simion Mbelwa Afisa mtendaji wa kata ya Utemini na mratibu msaidizi wa uchaguzi wa kata hiyo akitolea maelezo juu ya utaratibu wa uchukuaji wa fomu za kugombea nafasi ya udiwani  ( Picha na Doris Meghji)
Afisa mtendaji huyo wa kata ya Utemini amesema zoezi la uchukuaji wa fomu hizo umeanza rasmi  Agosti  08 mwaka huu na kutarajiwa kukamilika Agosti 21 mwaka huu majira ya saa 10 jioni kwa kila mgombea kutakiwa kudhaminiwa na wananchi wasiopungua 10   wenye vitambulisho za kupigia kura za uchaguzi mkuu huo wako kwenye daftari la kudumu la kupigia kura za uchaguzi huo kata ya Utemini.
Hii ni moja ya fomu za uteuzi wa ugombea wa nafasi ya udiwani na ubunge toka Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) wanazotakiwa uchukua na kuzijaza wateuliwa wa nafasi hizo za ubunge na udiwani wa vyama vyao katika ofisi za waratibu wasaidizi wa uchaguzi mkuu huo kwenye ofisi za halmashauri na ofisi za watendaji wa kata nchini.( Picha na Doris Meghji)
Hata hivyo katika zoezi la kutafuta wadhamini watakao mdhanini mgombea huo kwa nafasi ya udiwani kwa CCM kata ya Utemini Daftari limeonyesha ni wapiga kura 2460 ndio walioko kwenye daftari hilo la kudumu la wapiga kura  huku wapigakura 2807 hawako kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.Kata ya utemini iliandikisha jumla ya wapiga kura 5267 katika zoezi hilo mwaka huu.
Hili ni moja la daftari la kudumu la wapiga kura kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 Mwaka huu ( Picha na Doris Meghji)

MWISHO


Wednesday, August 12, 2015

WIKI YA USALAMA BARABARANI NA DRAGON EYE ( SPEED RADER) MWIBA KWA MADEREVA WA MAGARI

Na, Doris Meghji Jumatano Agosti 12, 2015
Singida
RPC  mkoa wa Singida  SACP Thobias Sodeyeka na RTO mkoa wa Singida wakiwa tayari kwa ajili ya kuzindua  maadhinisho ya wiki ya usalama barabarani  eneo la standi ya  basi ya kenda mikoani ( Picha na Doris Meghji) 
Wiki ya nenda kwa usalama bara barani yazinduliwa rasmi jana mkoani singida ikiwa na kauli mbiu ya Endesha salama okoa maisha kwa  kuwasii  wananchi  na watumiaji wa barabara  mkoa wa Singida kujitokeza kwa wingi kutembela maonyesho mbali mbali yatakayoendeshwa katika wiki hilo lengo ni kuwapatia elimu ya sheria za barabarani  kwa wananchi wa mkoa wa Singida
 
SACP Thobias Sodeyeka Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Singida kiongea kweye uzinduzi wa wiki ya usalama barabarani pembeni ni Mkuu wa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Singida (RTO) eneo la standi ya mabasi ya mikoa (Picha na Doris Meghji)
Kamanda wa jeshi la polisi  mkoani hapa SACP Tobias Sodeyeka amewataka wanachi hao kufika na kutembelea maonyesho hayo ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani ili waweze kupata elimu itakayoweza kuwasaidia kujua sheria za barabarani kwa wananchi wa mkoa wa Singida na wajibu wa kila mtumia barabara hizo.
Ni  baadhi ya vijana waliojitokeza kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani standi ya mabaisi ya mikoa wakifuatilia maelezo juu sheria za usalama barabarani ( Picha na Doris Meghji)
Kamanda huyo ametolea maelezo juu ya ajali za pikipiki zilizoweza kutokea na kupoteza maisha ya wananchi wa mkoa huo, katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu ni vifo 18 na majeruhi 8 vimetokea kwa kuwataka wananchi hao kufika katika maonyesho hayo ili kupata elimu ya sheria za usalama barabarani kwa kuwa waendesha piki piki ndio wanaongoza kwa ajali na kusababisha vifo mkoani hapo.
  Wananchi wa manispaa ya Singida wakifuatilia na kusikiliza maelezo toka kwa afisa wa polis kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya waiki ya usalama barabarani jana standi ya mabasi ya mikioni ( Picha na Doris Meghji)
 Kwa hiyo amewashauri  waendesha pikipiki ni vema wafike hapo na kupata elimu 


“We mwendesha piki piki  usalama wako kwanza ,ni mambo gani yanasababisha  kutokea kwa ajali hasa piki piki? kwanza hatuvai helmet,upakiaji kwa njia ya hatari, unapakia watu wanne na kile kiti cha pikipiki ni kidogo na ninafahamu  matatizo Sunlag huwezi kukata kona kwa haraka na kitu kingine ni kupatikia mizigo, unapakia watu huku umebeba mizigo na wakati mwingine ni huwa umelewa asubuhi tu umekwisha kunywa viroba hii ina hatarisha maisha yetu pindi ajali ikitokea ni vyema mje hapa mkapata elimu.” amewashauri wananchi hao kufika katika maonyesha hayo kamanda Sodeyeka.
Ni baadhi  ya maafisa wa jeshi la polisi kitendo cha usalama barabarani wakiwa katika eneo la uzinduzi wa wiki ya usalama barabarani  standi ya mabasi ya mkoa wa Singida maadhimisho hayo ( Picha na Doris Meghji)
Hata hivyo katika maonyesho hayo kupitia kitendo cha usalama barabarani  wa jeshi hilo la polisi  afisa G233 PC Phaston alitolea maelezo juu ya kifaa cha  kisasa cha upimaji wa mwendo kasi  ulevi wa madereva wa magari yakiwa barabarani chenye uwezo wa kupiga picha ya dereva,gari kwa ujumla na namba ya gari na mwendo kasi kwenye uzinduzi huo
Ni  G233 PC Phaston afisa wa usalama barabarani akionyesha na kutolea maelezo juu ya kifaa cha kisasa cha jeshi hilo cha kupima mwendo kasi wa gari na dereva akiwa barabarani   jana standi ya mabasi ya mkoa wa Singida kwenye uzinduzi wa wili ya usalama barabarani ( Picha na Doris Meghji)
Aidha katika kulezea kifaa hicho kwa jina la Dragon EYE amesema jeshi la polisi lina jumla ya vifaa hivyo vya kisasa 18 kwa mkoa huo lengo likiwa ni kuondoa utata uliokuwepo wa madereva kukataa mwendo wa gari lake na kudai kuwa amesingiziwa kwa kuwa kifaa hicho kinauwezo wa kupima gari liliko umbali wa kilomita moja na mita mia nane.  Ameeleza PC Phaston.
 
Ni standi ya mabasi ya mkoa wa Singida mabasi yakiingia jana  na kutoka wakzati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama mkoani Singida  na kueleea mikoa ya kaskazini na Magharibi ya Tanzania ( Picha na Doris Meghji)
Maashimisho hayo ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yamezinduliwa rasmi na rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mkoani Tanga na  ufungaji wa maadhimisho hayo ni Agosti 18 mwaka huu
 
Ni S/SGJ Paul David Afisa wa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani akitolea maelezo alama za barabarani ikiwa ni moja ya uelimishaji wananchi juu ya alama hizo wakiziona barabarani kwa watumiaji wote wa barabara mkoani Singida katika maadhimisho ya uzinduzi rasmi wa wili hiyo mkoani Singida ( Picha na Doris Meghji)



Wednesday, August 5, 2015

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII LAZARO NYALANDU ASHINDA KWA KISHINDO KATIKA UCHAGUZI WA KURA ZA MAONI NDANI YA CCM JIMBO LA SINGIDA KASKAZINI


 Na, Doris Meghji Jumatano  Agosti 05,2015
Singida
Katibu wa CCM wilaya ya Singida Vijijini Mwanamvua Killo akisoma matokeo ya uchaguzi wa kura za maoni ya ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Singida kaskazini mbele ya waandishi wa habari (Picha na Doris Meghji)
Matokeo jimbo la Singida kaskazini

 Waziri wa maliasili na utalii  Lazaro Nyalandu aibuka mshindi katika kinyang’anyiro cha kura za maoni  za uchaguzi wa ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi jimbo la Singida Kaskazini Mkoani Singida
 Lazaro Nyalandu Mshindi katika kinyang'anyiro cha nafasi ya ubunge jimbo la Singida kaskazini akijibu  maswali toka kwa waandishi wa habari mkoa wa Singida ( Picha na Doris Meghj
Akitangaza matokeo hayo Katibu wa CCM na Mratibu wa uchaguzi wilaya ya Singida vijijini jimbo la Singida Kaskazini Mwanamvua Killo amemtaja mgombea Lazaro Samweli Nyalandu kuwa mshindi katika uchaguzi huo kwa kupata kura 13,738 kati ya idadi ya kura 25,403 ya kura halili zilizopigwa na kura 43 zilizo halibika  kwenye uchaguzi huo akifutiwa na mgombea Justine Josephat Monko kwa kupata kura 5648 kwenye kinyang’anyiro hicho jimboni humo.
Mgombea Lazaro Nyalandu akipunga mkono mara baada ya kutangazwa mshindi kwenye kinyang'anyiro cha ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Singida kaskazini huu akimshikilia mkewe Faraja K. Nyalandu nje ya jengo la CCM mkoa wa Singida ( Picha na Doris Meghji)

 Katibu huyo amemtangaza rasmi Mgombea Lazaro Samweli Nyalandu kuwa ndio mshindi katika uchaguzi huo wa kura za maoni na kuwa ndiye mgombea atakayeipeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi mkuu  utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Hii ndio karatasi ya matokeo ya uchaguzi wa kura za maoni kwa nafasi ya ubunge jimbo la Singida kaskazini ( Picha na Doris Meghji)
 Katika kinyang’anyiro hicho jumla ya wagombea nane walijitokeza kuwania nafasi hiyo Nyalandu akiwa mmoja wa wagombea,  ambao ni Michael Athuman Mpompo aliyepata kura 3,501, Kura 730 zilikuwa za mgombea Mungwe ABC Athuman,Saba saba ni mgombea aliyepata kura 618, wakati mgombea Aron Yesaya Mbogho amepata kura 446,Amos Jilili Makiya amepata kura 425 na mgombea Yohana Elia Sintoo kapata kura 254 kwenye uchaguzi huo wa kura za maoni ya nafasi ya ubunge jimbo la Singida Kaskazini.
 Ni Faraja Kota Nyalandu akipongwezwa na wanaccm mara baada ya mume wake Lazaro Nyalandu alipotangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi wa kura za maoni ya nafasi ya ubunge jimbo la Singida Kaskazaini ( Picha na Doris Meghji)

 Naye mgombea Lazaro Nyalandu amewashukuru wanachama wa chama hicho kwa kumuamini na kumpa tena ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi huo mkuu wa kumchagua rais, mbunge na diwani katika serikali ya awamu ya tano jimboni humo.
Katibu wa CCM wilaya ya Singida vijijini Mwanamvua Killo akitolea maelezo juu ya utaratibu wa wagombea wakikataa kusaini matokeo wanatakiwa wafanye nini mbele ya waandshi  habari mara baada ya kutangaza matokeo ( Picha na Doris Meghji)
Katika kujibu moja ya swali toka kwa waandishi wa habari juu ya wagombea wenzake kwa kutosaini matokeo ya uchgauzi huo  Nyalandu  amesema suala la kutosaini matokeo ya uchaguzi kwenye uchaguzi huo imekuwa hiyo sio habari mpya bali ni kutokukomaa kisiasa kwa sababu uchaguzi huo umesimamiwa  kanuni na kwa kufuata katiba ya chama hicho.
 Lazaro Nyalandu Mshindi katika kinyang'anyiro cha nafasi ya ubunge jimbo la Singida kaskazini akijibu  maswali toka kwa waandishi wa habari mkoa wa Singida ( Picha na Doris Meghji)
“ Mimi nimekuwa mbunge kwa miaka  kumi na mitano hawakuwai  kusaini matokeo na niliendelea kuwa mbunge tu kwa hiyo sio habari mpya ni kutokukomaa kisiasa.” Asema Mgombea Nyalandu
Huyu ni Lazaro Nyalandu Mshindi katika kinyang'anyiro cha nafasi ya ubunge jimbo la Singida kaskazini akijibu  maswali toka kwa waandishi wa habari mkoa wa Singida ( Picha na Doris Meghji)
“sisi sote tumefanya kampeni vizuri na kwa vyovyote vile mshindi ambaye Lazaro Nyalandu ameshinda kididea mtu anayenifuata hata wakiunganisha  kura za wagombea wote wanane wakaamua tumpe mwenzetu mmoja ashinde bado hata shinda naamini aidha watafikiria wasaini au watakomaa kisiasa. lakini  hapa CCM mbele kwa mbele Nyalandu mbele kwa mbele na tunategemea wapinzani waisome namba”.Nyalandu asemea jambo hilo
Mgombea Mh. Lazaro Nyalandu na mkewe Faraja Nyalandu akiwa tayari kuwasalimia na kuwashukuru wanaccm waliomchagua na kushinda kwenye nafasi hiyo ya ubunge jimbo la Singida kaskazini ( Picha na Doris Meghji)
Hata hivyo jimbo la singida kaskazini  ni moja kati ya majimbo nane ya mkoa wa Singida mengine ni Singida mjini,Ikungi magharibi ,Ikungi mashariki,Iramba, Mkalama Manyoni Magharibi na Manyoni Mashariki

Mwisho.