Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Thursday, July 30, 2015

MWIGULI NCHEMBA AKANUSHA TUHUMA ZA TAKUKURU KUKIUKA SHERIA ZA TAASISI HIYO NA SHEREIA ZA UCHAGUZI

Na, Doris Meghji  Alhamis  Julai 30,2015
Singida
Katikati ni Mwigulu Nchemba na kushoto ni mwandishi wa habari Nathaniel Limu siku ya kumpokea Dkr. John Pombe Magufuli aliyopita kusalimia wananchi na wanachama wa CCM mkoa wa Singida ( Picha na Doris Meghji)
Naibu waziri wa fedha  na mgombea ubunge wa jimbo la Iramba  Mwigulu Nchemba amekanusha jana tuhuma zinazomkabili toka Tasisi ya kuzia na kupambana na rushwa  siku  baada ya taasisi hiyo kutoa taarifa kwa mgombea huyo kukiuka sheria ya TAKUKURU na  sheria ya gharama za uchaguzi mkoani Singida
Ni baadhi ya wagombea wa jimbo la Iramba Magharibi wakitoa malalamio yao kwa waandishi wa habari juu ya mgombea  Mwigulu Nchemba ( Picha na Doris Meghji)
Mh, Nchemba amekanusha tuhuma hizo mbele ya waandishi wa habari kwa kusema yeye ajakiuka sheria hizo  kwa kuwa tuhuma hizo zimeelekezwa kwenye ujenzi wa barabara unaoendelea wilayani hivyo amesema yeye hausiki na ujenzi huo.
Ni Mwigulu Nchemba akikaribishwa na naibu katibu mkuu bwana Luwavi  kusalimia wananchi wa mkoa wa Singida kipindi mgombea wa nafasi ya urais  John Pombe Magufuli akipita kujitambulisha mkoani singida akiwa safarini toka kanda ya ziwa kelekea Dodoma (Picha na Doris Meghji)
“mimi sina utamaduni wa kutoa rushwa, nina  uwezo wa kushinda hata bila kupiga kupiga kampeni,hivyo shughuli za kijamii haziwezi kuachwa kutekelezwa eti kwa sababu  wagombea wako kwenye kampeni alisisitiza” Mgombea Nchemba mbele ya waandishi wa habari.
Lazaro Nyalandu mgombea ubunge jimbo la Singida Kaskazini akiongea na waandishi wa habari jana mara baada ya wagombea wenzake wakimtuhumu kutopanda gari mmoja kwenye kampeni za kura za maoni za CCM mkoani Singida (Picha na Doris Meghji)
Naye mgombea wa jimbo la Singida kaskazi Lazaro Nyalandu amekanusha kuhusu tuhuma zilizotolewa na wagombea wenzake  juu yake ya kuto ongozana kutopanda gari moja na wagombea hao kama walivyokubalina  kwenye mikutano ya kampeni.
Baadhi ya wagombea wa jimbo la Singida kaskazini wakiwa tayari kwa ajili ya kuanza kampeni jimboni humo mara baada ya kikao na katibu wa CCM mkoa  ( Picha na Doris Meghji)
“Sijawahi kuona  genge la watu waliokuwa wazushi kama  baadhi ya watu na nao gombea nao wanatunga uongo, wanyaturu wanasema muongo apotelee mbali Mchawi aje nyumbani na mi nadhani sio vizuri kuivamia CCM wanatanga tanga sana kwamba mtu mwingine anachelewa, anaayewahi, kwa kweli watu dailili ya kushindwa ndio hiyo lakini wasubiri tarehe moja nawakikisha ushindi wangu utakuwa mnono ushindi wangu utakuwa wa kishindo kwa kazi nilizofinya na zilizotukuka katika miaka hii. 

Hivyo tarehe moja wagombea wote wanaogombea na mimi watapaka kura chini ya asilimi 10. ushindi ni kwangu ”.alisema Mgombea Nyalandu
 
Lazaro Nyalandu mgombea ubunge jimbo la Singida Kaskazini akiongea na waandishi wa habari jana mara baada ya wagombea wenzake wakimtuhumu kutopanda gari mmoja kwenye kampeni za kura za maoni za CCM mkoani Singida (Picha na Doris Meghji)
Hata hivyo katibu wa CCM mkoa wa Singida Bi Mary Maziku amewataka wagombea hao kutovunja kanuni utaratibu za chama hicho  hasa  kuhusu suala la wagombea kutoa msaada kipindi ni kosa hata kama aliahaidi toka siku nyingi ni kusitiza zoezi hilo hadi kipindi kura za maoni ndani ya ccm kukamilika.
Mwisho



No comments:

Post a Comment