Na, Doris Meghji Alhamis Julai 30,2015
Singida
Naibu waziri wa fedha na mgombea ubunge wa jimbo la Iramba Mwigulu Nchemba amekanusha jana tuhuma zinazomkabili toka Tasisi ya
kuzia na kupambana na rushwa siku baada ya taasisi hiyo kutoa taarifa kwa
mgombea huyo kukiuka sheria ya TAKUKURU na sheria ya gharama za uchaguzi mkoani Singida
Ni baadhi ya wagombea wa jimbo la Iramba Magharibi wakitoa malalamio yao kwa waandishi wa habari juu ya mgombea Mwigulu Nchemba ( Picha na Doris Meghji) |
Mh, Nchemba amekanusha tuhuma hizo mbele
ya waandishi wa habari kwa kusema yeye ajakiuka sheria hizo kwa kuwa tuhuma hizo zimeelekezwa kwenye
ujenzi wa barabara unaoendelea wilayani hivyo amesema yeye hausiki na ujenzi
huo.
“mimi sina utamaduni wa kutoa rushwa, nina
uwezo wa kushinda hata bila kupiga kupiga
kampeni,hivyo shughuli za kijamii haziwezi kuachwa kutekelezwa eti kwa sababu wagombea wako kwenye kampeni alisisitiza”
Mgombea Nchemba mbele ya waandishi wa habari.
Naye mgombea wa jimbo la Singida kaskazi
Lazaro Nyalandu amekanusha kuhusu tuhuma zilizotolewa na wagombea wenzake juu yake ya kuto ongozana kutopanda gari moja na wagombea hao kama walivyokubalina kwenye mikutano
ya kampeni.
Baadhi ya wagombea wa jimbo la Singida
kaskazini wakiwa tayari kwa ajili ya kuanza kampeni jimboni humo mara baada ya
kikao na katibu wa CCM mkoa ( Picha na
Doris Meghji) |
“Sijawahi kuona genge la watu waliokuwa wazushi kama baadhi ya watu na nao gombea nao wanatunga
uongo, wanyaturu wanasema muongo apotelee mbali Mchawi aje nyumbani na mi
nadhani sio vizuri kuivamia CCM wanatanga tanga sana kwamba mtu mwingine anachelewa, anaayewahi, kwa kweli watu dailili ya kushindwa ndio hiyo lakini wasubiri tarehe
moja nawakikisha ushindi wangu utakuwa mnono ushindi wangu utakuwa wa kishindo
kwa kazi nilizofinya na zilizotukuka katika miaka hii.
Hivyo tarehe moja wagombea wote wanaogombea na mimi watapaka kura chini ya asilimi 10. ushindi ni kwangu ”.alisema Mgombea Nyalandu
Hivyo tarehe moja wagombea wote wanaogombea na mimi watapaka kura chini ya asilimi 10. ushindi ni kwangu ”.alisema Mgombea Nyalandu
Lazaro Nyalandu mgombea ubunge jimbo la Singida Kaskazini akiongea na waandishi wa habari jana mara baada ya wagombea wenzake wakimtuhumu kutopanda gari mmoja kwenye kampeni za kura za maoni za CCM mkoani Singida (Picha na Doris Meghji) |
Hata hivyo katibu wa CCM mkoa wa Singida
Bi Mary Maziku amewataka wagombea hao kutovunja kanuni utaratibu za chama hicho
hasa kuhusu suala la wagombea kutoa msaada kipindi
ni kosa hata kama aliahaidi toka siku nyingi ni kusitiza zoezi hilo hadi kipindi
kura za maoni ndani ya ccm kukamilika.
Mwisho