Na, Doris Meghji Jumamosi Julai 25,2015
Singida
Wema Isaac Sepetu amepata kura 90 kati ya kura 490 ya kura
zilizopigwa na kushika nafasi ya nne jana akiwa
mmoja kati ya wagombea 13 wa ubunge wa viti maalum kwa tiketi ya Chama
cha Mapinduzi mkoani Singida
Mrembo huyo ambeya mwaka 2006 alikuwa
Miss Tanzania ameibuka na idadi kura
90 huku akimuacha mgombea anayemfuata
kwa tofauti ya kura 16 na kuwa wane kwenye kinyang’anyiro hicho kilichofanyika jana mkoani hapa. Katika uchaguzi huo kwa mujibu wa kipeperushi cha Mgombea huyo kimeeleza lengo la kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho ni kuleta maendeleo kwa wanawake wa mkoa wa Singida ikiwa ni pamoja na kuinua vipaji kwa vijana na wanawake ili wasijibweteke wajitume kwa nia ya kuweza kupata ajira ilio sahihi
Wema Sepetu akiwa na Katibu wa UWT
wilaya ya Ikungi Bi Yagi Kiaratu kabla ya mkutano kuanza mapema jana kwenye
ukumbi wa mikutano RC Mission ( Picha na Doris Meghji)
|
Aidha kimeleza elimu ya mgombea huo ni ya Shahada ya biashara ya kimataifa aliyoipata chuo kikuu cha Limkokwingi nchini Malasyia mwaka 2007- 2009
Elimu yake ya msingi na sekondari ameipata shule ya kimataifa (International Primary School ) ambapo shule ya msingi ni mwaka 1994 – 200 na sekondari mwaka International Secondary School) 2001 – 2006
Huku kuhusu uwanachama wake katika UWT ulianza mwaka 2009 ikiwa ni pamoja na uanachama wa UVCCM na Chama kwa ujumla alianza kuwa mwanchama mwaka huo wa 2009.
Wajumbe wa mkutano mkuu huo wa uchaguzi
wa wabunge viti maalum kwa mkoa wa Singida kuptia CCM katika ukumbi wa RC
Mission ( Picha na Doris Meghji) |
Wema Sepetu amewashukuru wajumbe wa mkutano huo mkuu na kuwaeleza kwamba safari yake ya siasa ndio kwanza imeanza na kuwataka waendeele kumuunga mkono katika eneo la siasa.
Bi Aysharose Matembe aimsaidia kumfunga
kitambulisho mgombea mwenzake Martha Gwau kabla ya uchaguzi kuanza katika
ukumbi wa RC Mission ( Picha na Doris Meghji) |
kwa mujibu wa uchaguzi huo walioibuka washindi katika uchaguzi huo wa wabunge wa viti maalum mkoani Singida ni Aysharose Matembe aliyepata kura 361 akifuatiwa na Martha Mlata kwa kupata kura 235 na hao kuwa ndio washindi katika kinyang'anyiro hicho.
Hata hivyo jumla ya wagombea kumi na tatu
wamejitokeza kugombea nafasi hiyo ya ubunge wa viti maalum na wagombea wawili
kutoka kitengo cha walemavu na NGO’s ambao ni Sarah A Mkumbo na Hawa Athumani Sengwa na kufanya idadi ya
wagombea kuwa 15 kwenye uchaguzi huo.
Wajumbe wa mkutano mkuu huo wa uchaguzi
wa wabunge viti maalum kwa mkoa wa Singida kupitia CCM katika ukumbi wa RC
Mission ( Picha na Doris Meghji) |
MWISHO.
No comments:
Post a Comment