Na, Doris Meghji Jumatano Julai 15,2015
Singida
Mgombea wa urais wa chama cha CCM
katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2015 Daktari John Pombe Joseph Magufuli ni
mbunge wa jimbo la Chato lililoko mkoa wa Geita na ni waziri wa ujenzi wa
Tanzania.
Alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1959
wilayani Chato Mkoani Kagera.
Kielimu, daktari Magufuli ana Stashahada ya elimu ya sayansi
akibobea kwenye masomo ya Kemia, Hisabati.
Mgombea huyo wa urais ana shahada
ya umahiri wa Sayansi na shahada ya uzamivu ya kemia.
Aidha daktari Magufuli amewahi kufundisha katika shule ya sekondari
Sengerema miaka ya themanini kisha akajiunga na mafunzo ya JKT .
Alizaliwa Oktoba 1959
Alipohitimu, daktari Magufuli na
aliaanza kufanya kazi katika kiwanda cha ‘Nyanza Cooperative Union akiwa Mkemia
kabla ya kuondoka hapo na kuwania ubunge.
Magufuli alianza mbio za ubunge
mwaka 1995 katika jimbo la Chato na kushinda kisha akateuliwa na Rais Benjamin
Mkapa kuwa naibu waziri wa Miundombinu.
Katika uchaguzi wa Mwaka wa 2000
pia aligombea ubunge na kushinda na Rais Mkapa akamteua kuwa Waziri wa
miundombinu.
Alianza siasa mwaka 1995
Katika uchaguzi wa mwaka 2005
daktari Magufuli aligombea ubunge kwa mara ya tatu na kupita bila kupingwa.
Rais Kikwete alimteua kuongoza
wizara ya Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi na baadaye akamhamishia hadi
wizara ya Mifugo na uvuvi. Mwaka 2010 alichaguliwa kuwa mbunge kwa mara ya nne
na Rais Kikwete alimrudisha katika Wizara ya Miundombinu na ujenzi.
Daktari Magufuli anachukuliwa kuwa ni mwanasiasa mwenye msimamo
thabiti, mchapa kazi na asiye yumbishwa au hata kufuata upepo wa kisaisa.
Anatambulika
kuwa Mchapa kazi
Watanzaniania wanamkumbuka kwa usimamizi na ujenzi wa barabara
na majengo thabiti.
Anakumbukwa kwa kuchukua hatua za kutoa amri za kubomolewa kwa
majengo ya kifahari ambayo alihisi yalikiuka sheria za ujenzi.
Na alipokuwa waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Bwana John Magufuli
alikwenda hadi bandari ya Dar-es-Salaam na kuizuia meli ya wachina iliyokuwa
inashukiwa kufanya uvuvi haramu katika sehemu ya bahari ya Tanzania.
MWISHO
No comments:
Post a Comment