Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Tuesday, July 28, 2015

TAKUKURU YAMSHIKILIA NAIBU WAZIRI WA FEDHA KWA TUHUMA ZA KUKIUKA SHERIA ZA GHARAMA YA UCHAGUZI MKOANI SINGIDA

Na, Doris Meghji  Jumanne Julai 28,2015
Singida

Katikati ni Mgombea Mwigulu Nchemba wakisalimiana na watu wakati Mh.  John Magufuli alipopita kusalimia  wanachama wa CCM kipindi akitoka kanda ya Ziwa keelekea Dodoma ( picha na Doris Meghji)
Taasisi ya kuzuia na kupambana rushwa mkoani singida inamshikilia na kumhoji Naibu waziri wa fedha Mh. Mwigulu Nchemba ambaye ni mmoja wa wagombea wa jimbo la Iramba  kwa tuhuma za kukiuka sheria za gharama za uchaguzi na sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11ya mwaka 2007 katika zoezi la kampeni za uchaguzi wa  kura za maoni zinazoendelea ndani ya vyama vya siasa nchini.
Kulia ni Mgombea  mwezake Mwigulu  Nchemba  Bwana Jairo wa jimbo la Iramba Magharibi akiwa na Mh.Diana Chilolo wakati Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM akipita usalimia wanachama wa CCM mkoa wa singida akitokea kanda ya Ziwa (Picha na Doris Meghji)
Akitoa taarifa hiyo kwa umma kwa waandishi wa habari mkoani hapa  mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Singida Joshua E. Msuya amesema  mnamo Julai 27 mwaka 2015 ofisi ya TAKUKURU mkoa wa Singida kupitia ofisi ya wilaya ya Iramba ilifanya mahojiano na Mh. Mwiguli Nchemba ambaye ni mmoja wa wagombea wa nafasi ya ubunge jimbo la Iramba magharibi kwa tiketi ya CCM  kwa tuhuma za kukiuka  sheria ya gharama za uchaguzi ya sheria ya kuzia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007  katika zoezi la kampeni za uchaguzi wa kura za maoni zinazoendelea ndani ya vyama vya siasa

Kwa mujibu wa Mkuu hiyo wa TAKUKURU  amewataadharisha wagombea wa nafasi za udiwani na wabunge mkoani singida kwa kutojihusisha  na vitendo vya rushwa kwenye kampeni za kura za maoni wakati wa uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba 2015  kwa kushawishi ili wachaguliwe kwa nafasi walizoziomba.

Aidha amesema kwa wale watakaobainika kukiuka sheria kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa kwa kutoa fedha,madawati,vifaa vya michezo,au rusha ya aina nyingine yoyote TAKUKURU itawafuatilia kwa karibu na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao kwa mujibu wa sheria  wa sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 mwaka 2007, sheria ya uchaguzi namba 343 R.E ikiwa ni pamoja na sheria ya gharama za uchaguzi namba 6 ya mwaka 2010.

Hata hivyo Kamanda Msuya ametaja kazi ya Taasisi hiyo ni kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa kwa kuelimisha kudhibiti uchunguzi na mashitaka.
Mwisho


No comments:

Post a Comment