Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Tuesday, July 21, 2015

UCHAGUZI WA MADIWANI WA VITI MAALUM KWA TIKETI YA CCM KUFANYIKA KESHO WILAYA YA SINGIDA MJINI

Na, Doris Meghji  Jumanne Julai 21,2015
Singida
Bi Leah Samike akikabidhi fomu ya kugombea ubunge viti maalum kwa tiketi ya CCM kwa  kaimu katibu wa UWT  Singida Mjini bi Zaituni Mlau ( Picha na Doris Meghji)
Jumla ya wagombea 23 wa nafasi ya udiwani wa viti maalum kwa tiketi ya CCM wamejitokeza kugombea nafasi hiyo  jimbo la Singida mjini huku zikiwa  zimebaki saa kadhaa tu zoezi la upigaji kura wa uchagua madiwani sita kati ya idadi hiyo iliyojitokeza kufanyika.
Bi Leah Samike akikabidhi fomu ya kugombea ubunge viti maalum kwa tiketi ya CCM kwa  kaimu katibu wa UWT  Singida Mjini Bi Zaituni Mlau ( Picha na Doris Meghji)
Idadi hiyo ya wagombea wa udiwani viti maalum imetolewa na kaimu katibu wa UWT wilaya ya Singida mjini Bi Zaituni Mlau  wakati wa urudishaji wa fomu za kugombea nafasi hiyo Julai 19 katika ofisi za UWT wilaya ya Singida mjini
 Baadhiingida mjini  ya wagombea wa nafasi ya udiwani viti maalum kwa tiketi ya CCM wilaya ya Singida mjini wakirudisha fomu kwa kaimu Katibu wa UWT wilaya ya Singida mjini Bi Zaituni Mlau ( Picha na Doris Meghji)

Katika zoezi hilo la upigaji kura wa kuwachagua madiwani wa viti maalum unaotarajiwa kufanyika kesho katika ukumbi wa mikutano VETA ndani ya manispaa ya Singida, ni madiwani sita tu ndio wanaohitajika kuchaguliwa miongoni mwa wagombea hao 23 ambao ni wa tatu kutoka tarafa moja na watatu kutoka tarafa nyingi zinazounda jimbo la Singida mjini

 Hata hivyo jimbo la Singida mjini lina tarafa mbili, Tarafa ya Unyakumi na Tarafa ya Mungumaji zenye jumla kata 18 ambapo theluthi moja ya idadi ya kata hizo ndio idada ya madiwani wa viti maalum wanaohitajika  kuwakilisha wanawake katika baraza la madiwani wa manispaa ya Singida

kwa upande wa wabunge wa viti maalum ni wagombea watatu wa nafasi ya ubunge wa viti maalum kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi wamerudisha fomu katika ofisi ya CCM wilaya ya Singida mjini

Wagomba hao ni Aziza Awadhi Ntandu,Leah Willium Samike na Sophia Josephin Nkungu ndio waliojitokeza kuchukua fomu na kurudisha za ubunge viti maalum kupitia chama hicho.
Bi Leah Samike akikabidhi fomu ya kugombea ubunge  wa jimbo kwa tiketi ya CCM  ofisi za CCM  wilaya ya Singida Mjini ( Picha na Doris Meghji)

Kwa mujibu wa mmoja wa wagombea wao Bi Leah Willium Samike amewashauri wanawake na waandishi wa habari kujitokeza na kugombea nafasi hizo ili nao waweze kuwa nauwakilishi mkubwa kwenye nafasi hizo  za maamuzi.
Bi Leah Samike akikabidhi fomu ya kugombea ubunge wa jimbo la  CCM kwa  katibu wa CCM   Singida Mjini Bi  Magdalena Ndwete  ( Picha na Doris Meghji)

Leah Samike akiwa mmoja  ya wagombea na  mwandishi wa habari aliyejikita katika upigaji  picha za kihabari amesema lengo la kugombea nafasi hiyo ni kuwasadia wananchi wa jimbo la singida kuwa na hali nzuri kiuchumi kwa kuimarisha uwezo wao kichumi katika sekta ya kilimo kupitia zao la alizeti, kwa kuanzisha viwanda vitakavyokamua alizeti hiyo ambapo itabadilisha na kukuza pato la mkulima wa zao hilo jimboni Singida.
Leah Samike akiwa ofisi za CCM wilaya ya Singida mjini tayari kwa kurudisha fomu za ugombea wa nafasi ya ubunge wa jimbo Singida mjini ( Picha na Doris Meghji)

Hii ikiwa ni pamoja na kuendeleza michezo kwa kuanzisha timu za watoto wa miaka sita hadi 12 ikiwa ni kuendeleza na kukuza michezo kwa wananchi wa jimbo hilo na taifa kwa ujumla
Katibu wa CCM wilaya ya Singida mjini Magdalena Ndwete akipokea fomu toka kwa mgombea ubunge Bi Leah Samike katika ofisi ya CCM singida mjini (Picha na Doris Meghji)

Mgombea Samike amewashauri waandishi wa habari kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi hizo za uwalilishi ili nao waweze kupaza sauti katika masual na changamoto mbali mbali zinazo wakabili wananchi wa tasnia hiyo ya habari katika utekelezaji wa majumukumu yao nchini.
 
Bi Magdalena Ndwete Katibu wa CCM wilaya ya Singida Mjini akitoa maelezo juu ya wagombea waliojitokeza kuchukua fomu na kurudisha kwa wakati za nafasi ya ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Singida Mjini ( Picha na Doris Meghji)
Hapa nakutana na katibu Bi Magdalena Ndwete wa CCM wilaya ya Singida mjini ananijuza juu ya akina nani waliojitokeza kutia nia na kufanikiwa kurudisha fomu hizo za ugombea kwa wakati.
Dada zake Leah Samike akiwa ofisi za CCM wilaya ya Singida mjini tayari kwa  kumsindikiza ndugu yao kurudisha fomu za ugombea wa nafasi ya ubunge wa jimbo Singida mjini ( Picha na Doris Meghji)

Katika kutolea maelezo suala hilo katibu wa CCM  wilaya ya Singida mjini  anataja majina ya watia nia 8 waliojitokeza kuwania nafasi hiyo ambao ni Hassan Philipo Mazara, Mussa Ramadhan Sima,Aman Adrew Rai,Leah Willium Samike, Philemon Joseph Kihemi, Ammhed Mohamed Athuman, Rajab Juma Mrao na Juma Ahhmed Kidabu
Leah Samike akiingia  ofisi za CCM wilaya ya Singida mjini tayari kwa kurudisha fomu za ugombea wa nafasi ya ubunge wa jimbo Singida mjini ( Picha na Doris Meghji)

Katibu wa CCM wilaya ya Singida Mjini Bi Ndwete amesema ni wagombea saba tu ndio waliofanikiwa kurudisha fomu hizo za  nafasi hiyo ya ubunge jimbo la Singida mjini.
Bi Magdalena Ndwete Katibu wa CCM wilaya ya Singida Mjini akipokea fomu ya Mgombea Leah Samike aliyegombea ubunge Jimbo la Singida mjini  kwa tiketi ya CCM Picha na Doris Meghji)
Katibu Ndwete alisema baada ya wagombea hao kurudisha fomu watakaa kikao pamoja na kamati ya siasa ya wilaya ya singida  mjini ili kuwapa maelezo na maelekezo  ya zoezi la kampeni lifanyike kwa wagombea kutakiwa kutotoa lugha za matusi na za kupakana matope  wakati wa kufanya kampeni zao ndani ya jimbo hilo
Bi Magdalena Ndwete Katibu wa CCM wilaya ya Singida Mjini akitoa maelezo juu ya wagombea waliojitokeza kuchukua fomu na kurudisha kwa wakati za nafasi ya ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Singida Mjini ( Picha na Doris Meghji)

Hata hivyo kikao hicho kimepunguza kiwango cha fedha za uchangiaji wa gharama za uchaguzi kutoka milioni 5 kwa kila mgombea hadi kufikia milioni 2.5 katika uchaguzi huo.
Leah Solomon  akiwa ofisi za  UWT  wilaya ya Singida mjini tayari kwa kurudisha fomu za ugombea wa nafasi ya udiwani wa viti maalum wilaya ya  Singida mjini ( Picha na Doris Meghji)
Upigaji kura za  maoni  za kuwachagua  wagombea wa nafasi ya ubunge  kwa tiketi ya CCM wa jimbo na madiwani wa kata unatarajiwa kufanyika Agosti Mosi mwaka huu, huku Leah Samike akiwa mgombea pekee wa kike  amejitokeza kugombea nafasi hiyo kwa tiketi ya chama cha mapinduzi.
MWISHO.





No comments:

Post a Comment