Na, Doris Meghji Ijumaa 1jumaa Julai 17, 2015
Singida - Ugombeaji Ubunge na udiwani
Bi Leah Solomon mgombea wa udiwani wa
viti maalum akikabidhiwa fomu na kaimu katibu wa UWT wilaya ya Singida mjini
Zaituni Mlau ofisi za jumuhiya hiyo ( Picha na Doris Meghji) |
Wanachama na makada wa chama cha Mapinduzi wamejitokeza
kwa wingi kuchukua fomu za kugombea nafasi za ubunge na udiwani mkoani Singida
Hii imejidhiirisha wazi leo siku ya pili
tangu chama hicho kianze kugawa fomu kwa watia nia ngazi ya ubunge na udiwani ambapo jimbo la singida mjini hadi muda majira
ya saa tano asubuhi huu ni watia nia
watatu ngazi ya ubunge wa jimbo la Singida mjini ambao ni Hassan Philipo
Mazara, Aman AP Rai na Mussa Ramadhan Sima hilo ni jimbo la Singida mjini
Bi Magdalena Ndwete katibu wa CCM wilaya
ya Singida mjini akiwa ofisini kwa ajili ya utoaji wa fomu za kugombea nafasi
ya ubunge jimbo la Singida mjini.( picha na Doris Meghji) |
Aidha kwa upande wabunge viti maalum kwa
jimbo la Singida kaskazini waliojitokeza kuchukua fomu ni Elizabeth Lucas
Kitiku,Martha Nehemia Gwau na Aysharose Ndogholi Mattembe huku watia nia kwa
nafasi ya udiwani viti maalum ni wanachama 17 wamejitoeza kuchukua fomu za
kugombea nafasi hizo kwa chama cha mapinduzi jimbo la Singida kaskazi.
Bi Magdalena Ndwete katibu wa CCM wilaya
ya Singida mjini akiwa ofisini kwa ajili ya utoaji wa fomu za kugombea nafasi
ya ubunge jimbo la Singida mjini.( picha na Doris Meghji) |
Wagombea mbali mbali walofika kuchukua
fomu za kugombea udiwani wa viti maalum wilaya ya Singida mjini katika ofisi ya
UWT Singida mjini (Picha na Doris Meghji) |
Zoezi hilo la uchukuaji wa fomu za
kugombea nafasi ya ubunge kwa upande wa jimbo Singida mjini ni shilingi 100,000/=
kwa wa ajili ya kulipia fomu huku hela ya mchango wa gharama za uchaguzi kuwa
shilingi milioni tano (5,000,000/=) ambazo licha ya kamati ya siasa ya wilaya
kupitisha kiasi hicho cha fedha kimeonekana kuwa kikwazo na tatizo kwa baadhi
ya watia nia wasio kuwa na uwezo mkubwa kifedha kugombea nafasi hiyo.
Katika kupata ufafanuzi juu ya mchango
huo wa uchaguzi kutoka kwa katibu wa CCM wilaya ya Singida mjini amesema
tuliache suala hilo la kuchangia gharama
za uchaguzi wa kuwa hadi sasa suala hilo ameiachia kamati ya siasa wilaya.
Zaituni Mlau kaimu Katibu UWT wilaya ya
Singida mjini akikagua kadi ya mmoja wa wagombea wa udiwani Viti maalum jimbo
la Singida mjini.(Picha na Doris Meghji) |
Nao madiwani viti maalum wilaya ya
Singida mjini zaidi ya watia nia kumi (10) wamejitokeza kuchukua fomu za
kugombea nafasi hizo udiwani jimbo la singida mjini ambapo Hadija Hassan Simba,Joyce John Sisha ,Mwandami
Rajab Kunde, Hamida Amri Said, Anisa Awadhi Mbaraka, Mwanaidi Ally
Njira,Mwahija Swalehe Abdalla, Mwajuma Husein Shaa,Leah Solomon Lisu na Margareth Malecela wamejitokeza
kuchukua fomu hizo za udwani viti maalum.
kwa upande wa wilaya ya singida mjini ambapo uchangiji wake ni shilingi elfu kumi ya fomu (10,000/-) na uchangiaji wa gharama za uchaguzi kuwa shilingi laki mbili (200,000/-) kwa kila mtia nia wa kugombea nafasi hizo ya udiwani wa viti maalum.
Kaimu katibu wa UWT wilaya yya Singida
vijijini Amina Omary akigawa fomu za kugombea ubunge na udiwani viti maalum jimbo
la Singida kaskazini (Picha na Doris
Meghji) |
kwa upande wa wilaya ya singida mjini ambapo uchangiji wake ni shilingi elfu kumi ya fomu (10,000/-) na uchangiaji wa gharama za uchaguzi kuwa shilingi laki mbili (200,000/-) kwa kila mtia nia wa kugombea nafasi hizo ya udiwani wa viti maalum.
Mmoja wa watia nia wa kugombea udiwani
viti maalum jimbo la Singida kaskazi akijaza fomu ya kugombea nafasi hio katika
ofisi ya UWT wilaya ya Singida vijijini (Picha na Doris Meghji) |
Aidha kwa mujibu wa kaimu katibu wa UWT
wilaya ya Singida mjini Bi Zaituni Hamis Mlau amesema katika zoezi amewaomba
wanachama wa UWT kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi hizo za maamuzi jimboni
humo.
Kaimu katibu wa UWT wilaya yya Singida
vijijini Amina Omary akimwelekeza mmoja wa watia nia ya udiwani viti maalum jimbo
la Singida kaskazini (Picha na Doris Meghji) |
Bi Amina Omary Adam ni kaimu katibu wa
UWT wilaya ya Singida vijijini ambapo jimbo la Singida Kaskazini linapatika
ametaja gharama za watia nia ngazi ya udiwani viti maalum wilayani humo uwa ni
shilingi 10,000/- kwa ajili ya fomu a kugombea nafasi na 200,000/- ni kwajili
ya gharama za uchaguzu kwa wagombea wapya kwa nafasi hiyo huku wagombea wa udiwani
wanaotetea nafasi zao kutakiwa kutoa elfu kumi ya fomu na kiasi cha shilingi
250,000/= kwa upande wa gharama za uchaguzi
Hata hivyo katibu huyo Amina Omary Adamu
amewaasa wanawake wajitokeze kwa wingi kuwania nafasi hizo za waamuzi kwa kuwa
ni zama za kidemokrasia kuchagua na kuchaguliwa ikiwa ni haki ya kikatiba kwa
chama hicho kuchagua na kuchaguliwa.
Zaituni Mlau kaimu katibu wa UWT wilaya ya
Singida mjini akikagua kadi ya mtia nia aliyefika kuchukua fomu ya uchaguzi (
picha na Doris Meghji) |
Utoaji wa fomu umeanza rasmi juzi Julai 15 na
kutarajiwa kukamilika Jumapili saa kumi kamili jioni Julai 19 mwaka huu
MWISHO.
Blog ipo pouwa keep it up
ReplyDelete