Na, Doris Meghji Jumatano Julai 15,2015
Nkungi - Mkalama
MNARA WA 3G WAAIRTEL ULIOZINDULIWA RASMI JULAI 12,2015 KIJIJI CHA NKUNGI WILAYANI MKALAMA (PICHA NA DORIS MEGHJI) |
Wananchi na wakazi wa kijiji cha Nkungi kata ya Mududa wilaya ya Mkalama mkoani Singida wameombwa kutumia vizuri fursa ya uwepo wa mnara wa mawasiliano toka kampuni ya
Airtel kwa huduma za mawasiliano na kiuchumi zinapatikana na kutolewa na
kampuni hiyo kwa maendeleo yao.
BAADHI YA WATEJA WA MTANDAO WA AIRTEL WAKIELEKEZWA KUJIUNGA NA MTANDAO HUO KIJIJINI NKUNGI WILAYA YA MKALAMA (PICHA NA DORIS MEGHJI0 |
Ombi hilo limetolewa na katibu tawala wa
wilaya ya Mkalama Benjamin Mwombeki jana kijijini Nkungi katika uzinduzi rasmi wa
mnara wa kampuni ya mawasilino
nchini Airtel kwa kuwataka wananchi hao
kutumia fursa ya uwepo wa mnara huo
kijijini hapo .
KATIKATI NI KATIBU TAWALA BENAJAMIN MWOMBEKI KUSHOTO NI VEO WA NKUNGI HUU KULIA NI MWENYEKITI WA SERIKALI YA KIJIJI CHA NKUNGI (PICHA NA DORIS MEGHJI) |
Kwa upande wa mwenyekiti wa serikali ya
kijiji cha Nkungi wilayani Mkalama Mohamed Idd Imbeve ametoa shukurani kwa
kampuni hiyo kuweka mnara huo kijijini hapo na kuomba kampuni ya Aitrel
kuboresha huduma ya Airtel Money ili kusadia watumiaji na wateja wa mtandao wa
simu wa kampuni hiyo kijijini Nkungi.
MSHEREHESHAJI AKIWAELEKEZA WANANCHI WALIOFIKA MNADANI HAPO SIKU YA UZINDUZI RASMI WA MNARA WA 3G KIJIJINI NKUNGI (PICHA NA DORIS MEGHJI) |
Awali akitoa maelezo kota kampuni hiyo
ya Airtel kwenye uzinduzi rasmi wa mnara
huo Mwakilishi wa Airtel toka Kanda ya
kati Hendrick Werner ameomba serikali ya kijiji na wananchi kuutumia mnara huo
katika nyaja ya mawasiliano kiuchumi bila kuusau kuulinda mnara huo ili uweze
kuwasidia kwenye shughuli hizo
BAADHI YA WATEJA WAKIUNGANISHA NA HUDUMA MBALI MBALI KWENYE SIMU NA LINE ZA MTANDAO WA AIRTEL KIJIJINI NKUNGI (PICHA NA DORIS MEGHJI) |
Mnara huo umezinduliwa hapo wenye uwezo
wa 3G wa kuhudumia wananchi wanaotumia
huduma hiyo kijijini hapo huo ni mmoja kati ya minara miwili iliyojengwa na
kampuni hiyo ya Simu kwenye wilaya ya mkalama ikiwa ni moja ya njia ya kusogeza
huduma ya mawasilino ya Simu karibu na wananchi mkoani Singida.
NI WANACHAMA SIKU YA MNADA WAKIWA TAYARI KUCHINGA NYAMA KWA AJILI YA NAMA CHOMA SIKU HIYO YA UZINDUZI WA MNARA WA 3G KIJIJINI NKUGI (PICHA NA DORIS MEGHJI) |
Katika uzinduzi huo jumla ya watumiaji
304 waliuganisha kwenye mtandao huo huku huduma mbali mbali za mtandao huo
ziliuwa ziitolewa za kuunganishwa kwenye mtandao,uuzwaji wa simu za promosheni
ikiwa pamoja na kuunganishwa huduma ya Aitel Money zimefanika kwenye uzinduzi
huo.
MNADA UIENDELEA HUKU SHUGHULI ZA UZINDUZI ZIKIFANYAKA SIKU HIYO NKUNGI (PICHA NA DORIS MEGHJI) |
kwa mujibu wa mtendaji na mwenyeiti wa kijiji hicho mnada huo kijijini Nkungi hufanyika kila tarehe 11 ya mwezi wilayani Mkalama.
Mwisho
No comments:
Post a Comment