Na, Doris Meghji Jumamosi Julai 26,015
Singida
Ni Aisharose Matembe na Martha Mlata
washindi katika uchaguzi huo wa wabunge wa viti Maalum kwa tiketi ya CCM mkoa
wa Singida ( Picha na Doris Meghji) |
Zoezi la kuwatafuta wabunge wa viti
maalum kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi
limekamilika leo mkoani singida huku Bi
AISHAROSE MATEMBE na MARTHA MLATA kuibuka washindi katika uchaguzi huo
uliofanyika leo katika ukumbi wa RC Mission manispaa ya Singida
Ni Aisharose Matembe na Martha Mlata
washindi katika uchaguzi huo wa wabunge wa viti Maalum kwa tiketi ya CCM mkoa
wa Singida ( Picha na Doris Meghji) |
Akitangaza matokeo hayo Msimamizi mkuu
wa uchaguzi huo Mkuu wa mkoa wa singida DR. Parseko Kone mara baada ya upigaji
kura wa kuwachagua wagombea hao katika
ukumbi huo wa RC Mission kwa kumtangaza Bi Aisharose Matembe mshindi kwa kupata
kura 361 akifuatiwa na Bi Martha Mlata ambaye amepata kura 235 wakati mgombea
Diana Chilolo amepata kura 186
Aidha katika uchaguzi huo ni wagombea
wawili tu ndio wanaohitajika kuwakilisha wanawake wa mkoa wa Singida katika
Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pindi chama cha mapinduzi kitashinda
kwenye uchaguzi mkuu wa wabunge wa majimbo na urais Oktoba 25 mwaka huu.
Msimamizi mkuu huyo ametaja majina
mingine ya wagombea waliogombea katika kinyang’anyiro hicho kuwa ni Wema Sepetu
kwa kupata kura 90,Sarah Mwambu kura 74, Martha Gwau kura 44, Rehema Madusa
kura 24, Aziza Ntantu kura 5, Mary
Kidundile kura 3, ikiwa ni pamoja na Leah Samike ambaye amepata kura 1 na
Elizabeth Lucas amepata kura 0 katika kinyanganyiri hicho.
Diana Chilolo mgombea na aliyekuwa
akitetea nafasi yake akiwashukuru wajumbe mara baada ya kusomewa matokeo ya
uchaguzi huo mkoani Singida ( Picha na Doris Meghji) |
Katika uchaguzi huo Diana Chilolo ambaye
ni Mwenyikiti wa UWT mkoa wa Singida na Mbunge wa viti maalum kwa vipindi
vitatu amewashukuru wajumbe hao na kuwapongeza washindi katika kinyang’aniro
hicho huku akiwataka wajumbe na wanccm kujiandaa vema na kuhaikisha Chama Cha
Mapinduzi kinashinda katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 ili wachaguliwa hao
waweze kuwakilisha vyema katika bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
kwa upande wa nafasi za wabunge wa viti maalum kupitia walemavu ni mgombea mmoja Bi Sarah Nalingigwa ndiye aliyegombea nafasi hiyo na kupata kura 489 ikiwa kura moja tu iliyoharibika katika uchaguzi huo.
Hata hivyo katika kuonyesha demokrasia
jumla ya wagombea 13 wamejitokeza kugombea nafasi hiyo ya ubunge wa viti maalum
ambapo mmoja wa wasanii maarufu nchini
Wema Sepetu amejitokeza kugombea nafasi hiyo kwa mwaka huu wa uchaguzi ndani ya
chama hicho mkoani Singida.
MWISHO
Wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa
wabunge wa viti maalum wa mkoa wa Singida wakiwa tayari kwa kusikiliza matoke
ya uchaguzi huo katika ukumbi wa RC Mission ndani ya manispaa ya Singida( Picha
na Doris Meghji)
Ni wasimamizi wa uchaguzi toka baraza la UWT mkoa wa Singida katika uchaguzi wa wabunge viti Maalum mkoa wa Singida ( Picha na Doris Meghji |
Wagombea wa uchaguzi huo wa
wabunge wa viti maalum kwa tiketi ya CCM mkoa wa Singida mara baada ya kupiga
kura tayari kwa kusomewa matokeo katika ukumbi wa RC Mission ( Picha na Doris
Meghji) |
Wema Sepetu wa pili kushoto na wagombea wenzake wa uchaguzi huo wa wabunge wa viti maalum kwa tiketi ya CCM mkoa wa Singida mara baada ya kupiga kura tayari kwa kusomewa matokeo katika ukumbi wa RC Mission ( Picha na Doris Meghji)
No comments:
Post a Comment