Na, Doris Meghji Jumatano Julai 08,2015
Singida
Huyu ndiye Mohamed Dewji Mbunge wa jimbo la Singida Mjini akisalimiana na baadhi ya wanachi waliojitokeza katika viwanja vya Peoples ( Picha Doris Meghji) |
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mohamed Gulam Dewji
ametangaz rasmi kutogombea tena nafasi ya ubunge katika kipindi hiki cha uchaguzi
kutokana na kuongezeka kwa majukumu
katika shuguli zake.
Tamko hilo ametoa leo katika viwanja vya
peoples ndani ya manispaa ya Singida mbele ya wananchi na wakazi wa jimbo kuwa
kutogombea kwake hakuta badilisha dhamira yake ya dhati ya kuliendeleza jimbo,
hivyo kupitia Mo Dewji foundation mambo mengi mazuri yatakuja.
Mheshimiwa Dewji amesema atakuwa tayari bega kwa bega kufanya kazi na kumuuonga
mkono kada yoyote atakeyeonyesha nia ya kugombea na kuchaguliwa na chama cha mapinduzi kugombea
nafasi hiyo ya ubunge jimboni Singida
Hata hivyo katika uongozi wake ameleta
na kupigania maendeleo mbali mbali kwa jimbo hilo hasa katika sekta ya Elimu Maji Afya na maendeleo ya jamii
Mohamed Dewji akihutubia wananchi na wakazi wa Singida ( Picha na Doris Meghji)
Mohamed Dewji amekuwa mbunge wa jimbo la
Singida mjini toka mwaka 2005 hadi 2015
Katika kutangaza kutogombea nafasi hiyo kamleta Msanii maarufu Diamond Platnum kutumbuiza na kuzikonga nyoyo za wakazi na wananchi za jimbo katika viwanja hivyo vya peoles.
MWISHO
No comments:
Post a Comment