Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Thursday, July 23, 2015

UCHAGUZI WA MADIWANI VITI MAALUM KWA TIKETI YA CCM WAKAMILIKA JANA JIMBO LA SINGIDA MJINI

Na, Doris Meghji  Alhamis Julai 23,2015
Singida
Rehema Shilla ndiye mgombea na ndiye akiyeongoza kwa kura za wagombea udiwani viti maalum jimbo la Singida Mjini akijinadi kwa wajumbe jana katika ukumbi wa VETA ( Picha na Doris Meghji)
Uchaguzi wa madiwani viti maalum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi jimbo la Singida umefanyika  jana huku Bi Rehema Shila  akiibuka kidedea kwa kupata kura 215 kati 276 za wajumbe wa mkutano huo mkuu wa uchaguzi jimboni humo.
Margareth Malecela akiomba kura na kujinadi mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa madiwani wa viti Maalum jimbo la Singida mjini ( Picha na Doris Meghji)
Katika uchaguzi huo jumla ya wagombea 22 wamejitokeza kugombea nafasi hizo za udiwani jimboni Singida ambapo madinwani 6 tu ndio wanaohitajika kuwalikisha wanawake katika baraza la madiniwani manispaa ya Singida
Ally Amanzi Mkuu wa wilaya ya Singida akiwaasa wanawake katika mkutano mkuu wa uchaguzi wa madiwani wa viti maalum kupitia CCM kwenye ukumbi wa VETA ( Picha na Doris Meghji)

Bi Rehema Shila ameongoza kwa kupata kura 215 akifuatiwa na Bi Margareth Malecela kwa kupata kura 197, Hadija Simba kura 186 Saidati Mziray kura 104  Angela Milembe 130 kura na Fatuma Makula  kapata kura 121 katika uchaguzi huo.
 

Margareth Malecela akiomba kura na kujinadi mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa madiwani wa viti Maalum jimbo la Singida mjini ( Picha na Doris Meghji)
Aidha katika uchaguzi huo ni wagombea wawili tu walitetea nafasi zao  za udiwani wa viti maalum ambao ni  Bi Margareth Malecela  kwa kura 197 na Bi Hadija Simba kupata kura  186  wakati Mwajuma Shaa  kapata kura 36 na Leah Solomo kapata kura 53   na kupoteza nafasi zao katika uchaguzi huo.

Bi Rehema Shila  na wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wakiserebuka kwenye ukumbi wa VETA kabla ya zoezi la upigaji kura kuanza  ( Picha na Doris Meghji)
Kwa upande wa mwenyekiti wa UWT wilaya singida mjini Bi Consolata Mziray  ameshindwa katika kinyang’anyiro hicho kwa kupata kura 19  kati ya hizo 276 za wajumbe wa mkutano mkuu huo wa uchaguzi.
Mgombea Mwajuma Shaa akipiga magoti kuomba kura kwa wajumbe wa mkutano mkuu huo wa uchaguzi wa madiwani wa viti maalum kwa tiketi ya CCM jimbo la Singida mjini ( Picha na Doris Meghji)


Naye mgeni rasmi katika uchaguzi huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano VETA Mkuu wa wilaya ya singida Ally Amanzi  amewaasa  wajumbe wa mkutano huo pamoja na wagombea wa nafasi hizo  kukubali matokeo kwa kuwa katika chaguzi zozote kuna mshindi na mshindwa na kutaka makundi yao yaeshe pale washindi watakapo patikana na kuwa wamoja.
Wajumbe wa kamati ya utekelezaji wa UWT wilaya ya Singida mjini wakiwa tayari kwa kusimamia  na kuchagua wajumbe na wagombea wa uchaguzi huo wa madiwa wa viti Maalum ( Picha na Doris Meghji)

Hata hivyo jana uchaguzi wa  madiwani viti maalum umefanyika wilaya za Mkalama, Iramba, Singida mjini na Singida vijijijini kwa wawakilishi hao kuchaguliwa mkoani Singida.
Angela Milembe katibu wa UWT mkoa wa Singida akiomba kura kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi katika kinyang’anyiro hicho cha udiwani viti maalum jimbo la Singida mjini katika ukumbi wa VETA ( Picha na Doris Meghji)
Consolata mziaray akiwa pamoja na wajumbe wa mkutano mkuu huo ( Picha na Doris Meghjji)
Hadija Hassani Simba akijinadai kwa wajumbe wa mkutano mkuu huo wa uchaguzi wa madiwani wa viti maalum ( Picha na Doris Meghji)

Leah Lisu akiomba kura kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi  wa madiwani jimbo la Singida mjini ( Picha na Doris Meghji)


MWISHO.






No comments:

Post a Comment