Na, Doris Meghji Jumatano Julai 29,2015
Singida
Hitaji la elimu ya upigaji kura miongoni mwa wanachama ndani ya vyama vya
siasa unahitajika kwa kujioonyesha wazi katika kampeni za kura za maoni
zinazendelea kwenye vyama hivyo nchini.
Hitaji limejionyesha kwenye moja ya mkutano wa kampeni za uchaguzi wa
kura za maoni za udiwani kwa tiketi ya
chama cha Mapinduzi tawi la Stesheni kata ya utemini mkoani Singida baada ya
mmoja wa wanachama wa chama hicho kuuliza juu ya utaratibu wa upigaji kura hizo
za maoni kwenye uchaguzi wa udiwani na ubunge utakaofanyika Agosti mosi mwaka
huu.
Aidha akijibu swali hilo juu ya
utaratibu wa upigaji kura siku hiyo ya uchaguzi Katibu wa itikadi na uenezi
wa CCM kata ya Utemeni Martin kahuka
amelekeza kwa wanachama hao wanatakiwa kuhakikisha wanakuwa na kadi zao za
uanachama wa CCM ikiwa ni pamoja na kitambulisho cha upigaji kura wa uchaguzi
mkuu utakofanyika Oktoba 25,2015.
Ni viongozi wa ccm kata ya utemini
wakiwasiiliza kwa makini wagombea wa nafasi ya udiwani wakijinadi kwenye
mkutano wa kampeni za kura za maoni mbele ya wajumbe ( Picha na Doris Meghji) |
kwa kuwa upigaji kura wa uchaguzi huo ni wa kura za maoni ndani ya chama chao.
Uchaguzi huo wa wabunge na madiwani wa
kura za maoni utafanyika Agosti Mosi mwaka huu kwa wanaccm kuwachagua wabunge
na madiwani wao watakao peperusha bendera ya CCM.
Kwa kusisitiza jambo hilo katibu huo wa
itikadi na uenezi amesema mwanachama anatakiwa kuwa na kadi hiyo ya uanachama
wa CCM na kadi ya kupiga kura ya uchaguzi mkuu ili pindi mgombea amtakaye mchagua
kupeperusha bendera ya chama hicho wawe na uhakika wa kupiga kura kwenye
uchaguzi mkuu wa rais,mbunge na diwani utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Hata hivyo katika kampeni hiyo ya kura
ya maoni kwa udiwani wa chama cha mapinduzi kata ya utemini ni wagombea wawili
tu ndio waliojitokeza kugombea nafasi hiyo ambao ni Bartazary Lessio Kimario na
Hanje Narumba Barnabas.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment