Na, Doris Meghji Jumatano Julai 15,015
Singida
Ugawaji
wa fomu za uchaguzi katika kugombea nafasi za uwakilishi wa wananchi ngazi ya ubunge na
udiwani umeanza leo ndani ya chama cha mapinduzi nchini
Hii ni fomu ya kugombea nafasi ya
udiwani ubunge kwa chama cha mapinduzi (Picha na Doris Meghji) |
Nikitembelea moja ya ofisi ya kata ya
chama cha Mapinduzi ndani ya manispaa ya Singida Kata ya Utemini nakutana na mmoja wa wagombea
nafasi ya udiwani Bartazary Kimario akichukua fomu katika kugombea nafasi hiyo udiwani
akiwa ni diwani anayeitetea nafasi yake.
Bartazary Kimario akijaza jina lake
katika kitabu cha kujiorodhesha cha watia nia katika kugombea nafasi ya udiwani
kata ya utemini leo ofisi za chama kata ya utemini (Picha na Doris Meghji) |
Aidha katika kupata maelezo juu ya
taratibu za kugombea nafasi hiyo katibu wa CCM kata ya Utemini Bi Mary Frank
amesema kugombea nafasi hiyo ya udiwani jumla ya shilingi laki tano na elfu
zinahitajika kutolewa na kila mtia nia wa kugombea nafasi hiyo kwa kiasi cha
shilingi elfu 10,000/= kwa ajili ya ada ya fomu huku shilingi 500,000/= ikiwa ni
mchango wa kampeni ya uchaguzi ndani ya chama hicho.
Amesema kila mtia nia wa nafasi hio ya
udiwani anatakiwa kuwa na wadhamini 25 wakiwa ni wanachama wa kawaida wa CCM
kutakiwa kumdhamini mgombea wa nafasi hiyo.
Mary Frank katibu wa CCM ata ya utemini
akimkabidhi fomu mtia nia Bartazary Kimario katika kugombea nafasi hiyo ndani
ya CCM leo katika ofisi ya kata (picha na Doris Meghji) |
Zoezi hilo la uchukuaji wa fomu hizo limeanza leo Julai 15 hadi Julai 19 saa kumi kamili jioni
Hii ni stakabadhi ya ada ya fomu ya
kugombea nafasi ya udiwani kwa tiketi ya
CCM (Picha na Doris Meghji) |
Hivyo amweataka wananchama na makada wa
CCM kujitokeza kugombea nafasi hiyo kwa kuwa ni haki ya kila mwanachama hai kikatiba wa
kata hiyo.
Hii ni stakabadhi ya mchango wa kampeni
ndani ya chama hicho katika ngazi ya nafasi ya udiwani (Picha na Doris Meghji)
|
Hata hivyo kata ya utemini ni moja kati ya kata 18 zinazounda
jimbo la singida mjini mkoani hapa.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment