Na, Doris Meghji Jumatatu Januari
20,2014
Singida
Watu kumi na tatu (13)wamefariki dunia
na mmoja kujeruhiwa leo majira ya saa mbili (2:00) asubuhi baada ya ajili iliyohusisha magari mawili gari la abiria la aina ya Noah na lory skania
eneo la kijiji cha Isuna wilaya Ikungi Mkoani Singida
askari wa usalama barabarani na foleni ya wananchi waliofika kutambua ndugu zao wakisubiri kuingia katika chimba cha mochwari hosptali ya mkoa wa Singida( Picha Na Doris meghji) |
Akiongea na waandishi wa habari Kamanda
wa Jeshi la Polisi Mkoa wa singida SACP
Geofrey Kamwela amesema ajali hiyo imetokea leo majira ya saa mbili asubuhi eneo la Isuna wilaya ya Ikungi ,kwa gari aina ya Lory scania yenye usajili namba
T.687 AXB mali ya Musa Transpot likitokea Mkoani Mwanza likiwa limebeba samaki
wabichi kugongana na uso kwa uso na gari
aina ya Noah yenye usajili namba T.730 .BUX mali ya Mbua Ndofu mkazi wa Ikungi likitoka
Itigi kuja Singida mjini na kusababisha vifo vya watu 13 na kujeruhi mtu mmoja katika
ajali hiyo
baadhi ya wananchi waliojitokeza kuja kutambua maiti za ndugu zao leo katika eneola mochwari hospitali ya mkoa wa singida (picha na Doris Meghji) |
Kwa mujibu wa kamanda Kamwela amesema chanzo
cha ajali hiyo ni mwendo kasi na uzembe wa madereva barabarani “katika kukagua tukio
inaonyesha ni uzembe, magari hayo wamekutwa upende mmoja wa barabara upende
wa gari aina ya Noah”alisema kamanda
Kamwela
Aidha katika kutiko hilo dereva gari
aina ya noah alifariki dunia hapo hapo huku dereva wa Lory Skania na utingo wake walikimbia na kuliacha lory hilo
Hata hivyo jeshi la polisi mkoani
Singida linatoa wito kwa wananchi wote wa mkoa huu na Tanzania kwa ujumla kwa
watumiaji wa barabara kuwa waangalifu hasa katika kipindi hiki cha msimu wa
mvua jambo ambalo husababisha ajali na kupoteza nguvu kazi,uharibifu wa vyombo
vya usafiri na miundo mbinu ya barabara
Jeshi la polisi linaendelea na kuwatafuta
derava na utingo wa lory hilo
Kwa upande wa mganga mfawidhi wa
Hospitali ya mkoa wa Singida (MOI) Daktari Joseph Malunda amesema hospitali ya mkoa imepoke leo majira ya 4:00 asubuhi maiti 13 na majeruhi mmoja.
Kwa mujibu wa Daktari, Malunda ametaja jina
la aliyejeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni Hamis Daud mwenye umri miaka 23 amelazwa katika hospitali hiyo ya mkoa na hali
yake enanedelea vizuri ambapo amekatika mkono wa kushoto na majereha kidogo
kichwani
mmoja ya maiti ya ajli hiyo katika chmba cha mochwari hospitali ya mkoa wa singida(picha na Doris Meghji) |
Kwa upende wa watu waliopoteza maisha amewataja kuwa ni Haji
Mohamed (29) mkazi wa msisi,Salma Omary Mkazi wa Itigi,Omary Shabani (44) mkazi
wa Itigi,Ramadhani Mianga Mkazi wa Sanjaranda,Athumani Kalemba (38) Mkazi wa
Mtukula,Matunku Rashid (68 ) mkazi wa Sanjaranda,Samiri Shabani (20) mkazi wa
Puma,Nyumumwi Omary (10) mkazi wa
Itigi,Swalehe Hassan (28) Mkazi wa sanjaranda,Florence Mwaleki Nkuwi (35) Mkazi
wa Ikungi,Devid Emmanuel Suleman (24) mkazi wa Sanjaranda,Martin Marco (38)
mkazi wa Itigi na mtoto mwenye umri wa miezi 4
Askari wa usalama barabarani wakichukua maelezo ya baadhi ya wanachi nje ya mochwari ya kutambua ndugu zao(picha na Doris Meghji) |
Daktari Malunda amesema katika maiti
hizo maiti 4 ni za familia mmoja ambapo baba,mama na mtoto wa miaka 10 na kichanga
cha miezi minne kimefariki dunia kutokana na ajili hiyo
Hivyo maiti zote kumi na tatu zimekwesha
tambulika na ndugu zao.
Mwisho
baadhi ya watu wakisubiri kuingia Mochwari ya hosptali ya mkoa kutambua maiti za ndugu zao( Picha na Doris Meghji) |
Baadhi ya aski wa jeshi la polisi wakiwa kazini kuchukua maelezo ya ndugu ya maiti ajali ya watu waliiofariki dunia leo(picha na Doris Meghji) |
No comments:
Post a Comment