Na, Doris
Meghji Jumatano 22,2014
Singida
Suala la
ongezeko la pato ngazi ya kaya laweza kuongezeka kwa baadhi ya wananchi wa mkoa wa
Singida hasa kwa wanawake ambao ndio walezi wakuu wa familia imefahamika.
Hayo
yamebainishwa wazi na Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari wanawake
(WMO) mkoani singida Bi Evarista Lucas wakati akifanya mahojiana blog hii bara
baada ya kupata ruzuku toka mfuko wa misitu Tanzania (TTF) Tanzania Forest Fund
kiasi cha shilingi million 10, kuwa chama chake kinatarjia kutoa elimu na
usaidia wanawake juu ya suala la
utunzaji wa misitu kupitia ufugaji nyuki katika vikundi vinne kwenye vijiji vya
wilaya ya Ikungi na Singida.
Bi Evarista Lucas Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari wanawake WMO mkoa wa singida akifanya mahojianao na karibusingida blog. |
Kwa mujibu
wa Bi Lucas amesema “wanawake na watoto ndio walengwa wakuu wa mradi huu, lengo
letu ni kuongeza pato la kaya kwa upande wa wanawake hivyo vikundi vinne kutoka
katika vijiji hivyo vinavyofuga nyuki tutavipatia mizinga ya kisasa 20 kila
kimoja ambapo wakitumia vizuri watavuna asali ya kutosha na watauza na kuongeza
kipato kwa kaya zao.alieleza Bi lucas
mmoja ya mzinga wa kisasa mtaalam akionyesha jinsi gani nyuki wakataa katika mzinga huo(picha na Doris Meghji) |
Aidha amesema
mradi huu unatarjiwa kuanza mapema mwaka huu hasa katika mwezi huu wa januari
ndio mwezi wa kutundika mizinga katika misitu hiyo ambapo baadhi ya vijiji vitakavyonufaika na mradi huo ni pamoja na kijiji cha Ilongero,Masweya na Ighombwe vyenye vikundi vya ufugaji nyuki.
Baadhi ya Mizinga ya kisasa katika msitu wa Agondi wilaya ya Manyoni Mkoani Singida (picha na Doris Meghji) |
Akisisitiza
juu ya utekelezaji mradi huo amesema utunzaji misitu na mazingira chama chake kitatoa elimu ya utunzaji mazingira na kufundisha mbinu mbadala za
ufugaji nyuki kwa kutimia mizinga hiyo ya kisasa na urinaji asali zisiozoharibu
mazingira wakati wa kurina.
Hata hivyo
kwa upande wa soko la asali amesema soko liko wazi kutokana faida na manufaa ya asali kwa
binadamu ambapo bei ya sasa ya lita mmoja ya asali ya nyuki wadogo ni shilingi 10,000/= huku lita ya nyuki wakubwa
ni shilingi 8000/= kwa lita.
Mwisho
No comments:
Post a Comment