Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Wednesday, January 22, 2014

MAUAJI NA MAJERUHI- YATOKEA JANA TARAFA YA MGORI - MKOANI SINGIDA



Na, Doris Meghji  Jumatano Januari 22,2014
Singida
Mtu mmoja ameuwawa jana na wengine kujeruhiwa  kutokana na ugomvi uliozuka katika  kijiji cha Nduamughanga kata Mughanga tarafa ya Mgori wilaya na Mkoa wa Singida 

Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida SACP Geofrey Kamwela amemtaja aliwawa katika ugomvi kuwa ni Athumani Jumanne Mkatapori (40) mkazi wa kijiji cha Nduamughanga ameuwawa vibaya kwa kukatwa katwa na mapanga sehemu za kichawani na mkononi na kuchomwa mshare mdomoni na watu wasiojulika kutoka katika kijiji cha Handa wilaya ya Chembe mkoani Dodoma.
 
SACP GEOFREY KAMWELA- KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOA WA SINGIDA AKITOA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI (picha na Doris Meghji)
Kamwela amesema, chanzo cha mauji hayo ni ugomvi uliozuka kati ya watu wasiojulikana idadi yao wakidai kurejeshewa ng’ombe 180 waliokamatwa baada ya kuingia kwenye hifadhi ya Msitu wa Mgori januari 20 mwaka huu,
ambapo watu hao walifika kijijini hapo na kuingia porini  walipokuwa wanakijiji hicho wakichunga na kuchukua ng’ombe 68 mbuzi 101 ,kondoo 6 na punda wa 3 mali ya Abraham Mohamed (60) na wenzake wakazi wa kijiji cha Nduamughanga na kutoweka wakidai kuwa ni fidia ya ng’ombe 180 walidhuwiliwa.

hivyo wanakijiji wa kijiji hicho walianza kufuatilia kurudisha  mifugo yao ndipo ugomvi huo ulipozuka na kusanabisha mauji ya Athuman Jumanne Mkatapori na marejuhi ya watu  17 wa kijiji cha ndumughanga
 
Kamanda Geofrey Kamwela akisisitiza jambo kwa wanahabari mara baada ya kutoa taarifa kwa vyombo vya habari Ofisini Kwake (picha Doris Meghji)
Kwa mujibu wa kamanda Kamwela amesema watu  waliojeruhiwa katika ugomvi huo ni Hamisi Ramadhani(36),Elisante Saidi (51) Omari Omari(42) Muna Hamis (38) Abrahamu Mhamed (60) Hanis Rajabu (33) Yohana Saidi (37)  na mtendaji wa kijiji hicho cha nduamughanga Mwaftari Rajabu (35).

Wakati wengine ni Ramadhani Rajabu (26) Msafiri Juma,Omari Hamis(33) Hamis Sharifu (32) Jumanne Musa (28) Abdi Musa,Daudi Karata na Helena Bakari wote wakazi wa kijiji hicho.

Amesema;  hali za majeruhi zinaendelea vizuri, wote wakitibiwa  katika kituo kidogo cha afya kilichopo kijijini hapo huku Elsante Saidi akiwa amelazwa hosptaili ya mkoa kutokana na kujeruhiwa vibaya katika ugomvi huo.

Aidha katika kufuatilia tukio hilo jeshi la polisi mkoani hapo linawashikilia watu wawili ambao ni Nicodemo Ako (45) mkazi wa kijiji cha Giiting Wilaya ya Hanang mkoani Manyara na Athumani Soa mkazi wa kijiji cha Handa wilaya ya Chemba mkoa wa Dodoma.
Baadhi ya Waandishi wa Habari akimsikiliza kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida (picha na Doris Meghji)



Hata hivyo jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na watuhumiwa watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika huku likitoa wito kwa raia wema kutoa ushrikiano kwa kutoa taarifa zinazohusiana na tukio hilo.
Mwisho

No comments:

Post a Comment