Jumatatu 13 Januari 2014
Abiria
28 wakiwemo watoto wanne wamejeruhiwa baada ya basi walilokuwa wamesafiria la
Kampuni ya Shabiby kugongana na Lori tupu la mafuta na kupinduka katika kijiji
cha Kisaki umbali wa kilometa 10 kwenye Barabara Kuu ya kutoka Mjini Singida
kwenda Dodoma.
Basi la Kampuni ya Shabiby likiwa limepinduka mara baada ya kugongana na gari la kusafirishia mafuta leo katika kijiji cha Kisaki katika manispaa ya Singida |
Taarifa
zilizopatikana kwenye eneo la tukio zimeelezwa kuwa Basi hilo lenye namba
T930BUW aina ya Yutong lililokuwa likiendeshwa na Dereva wake ambaye
amekimbia
mara baada ya ajali hiyo linakadiriwa kuwa na abiria wapatao 48 lilipata ajali
hiyo jana saa 6:50 mchana wakati lilipojaribu kulipita lori hilo upande wa
kulia .
Taarifa
hizo ambazo pia zimethibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida zinasema kuwa
kitendo hicho kilisababisha kuligonga Lori hilo RAA 496N aina ya MERCEDES BENZ
lililokuwa likitokea Mjini Kigali nchini Rwanda kwenda Dar es Salaam likiwa na
dereva wake Barimana Benjamini (37) na kuanguka upande wa kulia wa Barabara na
kujeruhi abiria28
Basi la kampuni ya Shabiby likiwa limepinduka na kuharibika vibaya sehemu ya mbele |
Baadhi ya abiria wakiwa hawajui la kufanya mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo eneo la kijiji cha Kisaki km 10 toka makao makuu ya Manispaa ya Singida |
MWISHO
No comments:
Post a Comment