Na Evarista Lucas
Singida
Jan 20,2014
Imeelezwa kuwa; watu kumi na watatu wamepoteza
maisha papo hapo mapema leo saa mbili za asubuhi katika ajali ya gari; ambapo gari aina ya Noah imegongana uso kwa
uso na lori la mizigo aina ya Skania.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo; kamanda wa
Polisi mkoani hapa bwana Geofrey Kamwela amesema; katika ajalihiyo iliyotokea
katika kijiji cha Isuna wilayani Ikungi mkoani Singida waliofariki ni abiria
kumi na watu kati yao mwanamke mmoja na binti wa miaka kumi.
Kamwela amesema
gari ya abiria aina ya Noah yenye namba T370 BUX mali ya Mbua Ndofu mkazi wa Ikungi; ikiwa na abiria kumi
na wanne akiwemo dereva wa gari ilikuwa ikitokea itigi kuja Singida mjini na
ndipo ilipokutana uso kwa uso na lori hilo lenye namba T 687 AXB mali ya Mussa transport lilokuwa
limetokea Mwanza likiwa limebeba samaki wa bichi.
Aidha; Kamwela amesema kuwa baada ya uchunguzi wa
ajali hiyo iliyotekea kwa uzembe katika
bara bara kuu ya Singida- Dodoma upande ambapo noah ilikuwa ikipita; imebainika
kuwa gari zote mbili zilikuwa katika mwendo kasi kutokana na uharibifu
uliojitokeza katika magari hayo ambapo Noah ilipita chini ya uvungu wa lori
hilo.
Mbali na hayo Kamwela ametoa wito kwa madereva wote
kuwa waangalifu katika kipindi hiki cha mvua ambapo bara bara zinakuwa na
utelezi na pia ukungu mwingi hali ambayo ni hatari kwani inaweza kusababisha
matatizo kwa binadamu na uharibifu wa
miundo mbinu.
Kwa upande mwingine; Jeshi la Polisi mkoani Singida
linaendelea kuwasaka dereva na utingo wa lori hilo ambao walitokomea
kusikojulikana mara baada ya ajali hiyo ili kujibu tuhuma zinazowakabili.
Kwa upande wake mganga mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Singida
Dokta Joseph Malunda amethibitisha kupokea miili ya marehemu hao kumi na watatu
na majeruhi mmoja Hamisi Daudi miaka 23
aliyesalimika katika ajali hiyo.
Malunda amesema kuwa majeruhi huyo aliyekuwa katika
Noah amekatika mkono wa kushoto na ana
majeraha katika kichwa; na kusema kuwa majeruhi huyo anendelea anaendelea vizuri na kuwa anaendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo.
Amewataja waliofariki katika ajali hiyo ni Salma
Omari(umri ha ukufahamika), Omary Shabani(44), Nyamumwi omari(10), motto mchanga
wa miezi mine, Martin Marko(30) wakazi wa Itigi mkoani hapa.
Wengine ni Devid Emanuel Suleman(24), Matunku
Rashid(68), Swalehe Hassan (28) wa Sanjaranda, Athuman Kalemba(38) wa
Kyaka Mutukula, Jaji Mohamed (29) wa
Msisi, na Samir Shaban (20) wa Puma.
MWISHO
INAUMIZA KWA KWELI NA NI PIGO KUBWA KWA MKOA WA SINGIDA. TUNAWAPA POLE WAFIWA WOTE MUNGU AWATIE MOYO
ReplyDelete