Na Evarista Lucas
Singida,
Jan 20,2014
Wito umetolewa kwa viongozi wa kidini kuwa na
mawasilano mazuri kuanzia ngazi ndogo ya jumuiya ndogo ndogo hadi ngazi ya
uongozi wa juu ili kuimarisha utendaji kazi katika kumtangaza Kristo.
Wito huo umetolewa mapema jana na paroko wa parokia
ya Moyo Mtakatifu wa Yesu, Jimbo Katoliki la Singida; Padri Jonas Mlewa wakati
akitoa neon la shukrani kwa niaba ya mapadri wa Parokia hii katika hafla fupi ys
kuwapongeza kwa utume wao.
Mlewa amesema; mawasiliano ndiyo yanayopelekea utendaji kazi kuwa
mwepesi na kazi kuonekana nzuri na kuwaasa vioongozi kuondoa mwanya wa
mawasiliano kuanzia ngazi ya Jumuiya ndogo ndogo hadi kwao mapadri.
Sanjari na hayo Mlewa ameongeza kusema kuwa kwa kitendo kilichooneshwa na viongozi hao wa
kidini si tu kuutambua uwepo wao kama watenda kazi katika shamba la bwana; bali
ni neno lile lisemalo “Hii ndio siku aliyoifanya Bwana, tufurahi na
tuishangilie…”
Ameongeza kusema kuwa mapendo yana nguvu kuliko mauti
na kwamba mtu akipenda hakuna kinachomshinda na kusisitiza kuwa huo ndio upendo
waliokuwa nao hao viongozi kwa kutenga siku hiyo maalumu kuwapongeza mapadri
hao.
Mbali na hayo Mlewa amewataka viongozi wa Jumuiya
ndogo ndogo kuwaamsha wale waliolala katika imani na kushindwa kuhudhuria
jumuiya ndogo ndogo. Huku akiwataka viongozi wa jumuiya kuhakikisha kuwa kila
jumuiya inakuwa na daftari ya mahudhurio ili kuwajua wale wasiohudhura.
Kwa upande mwingine; Makamu Mwenyekiti wa Parokia ya
Moyo Mtakatifu wa Yesu jimboni Singida bwana Abel Nyaswa amewaasa wazazi na watu
wengine kuepuka kuwawekea vikwazo vijana
wanaopenda wito wa upadri na utawa ili kuongeza watenda kazi jimboni
hapa.
Amesema; badala ya kuwavunja moyo vijana hao, wazazi
na walezi hawanabudi kuwatia moyo vijana hao ili waweze kuyafikia malengo
waliojiwekea na hatimae kanisa lijivunie kwa kupata matunda hayo.
Ameongeza kusema kuwa hafla hii leno lake ni kuweza
kuwasaidia mapadri wa Parokia hii waweze kupata mahitaji yao muhimu kama
ilivyoazimiwa katika mkutano mkuu wa kichungaji mnamo mwaka 2008.
Aidha ; Nyaswa amesema kuwa licha ya maadhimisho
haya kutokufanyika toka ilipoazimiwa miaka sita iliyopita; amesema kuwa kitendo
hicho ni cha shukrani kwa viongozi hao wa kiroho na kuwa kiwe cha kumtolea
Mungu shukrani kwa mema aliowajalia na na kujenga ukaribu na vioongozi wao wa
kiroho.
Ingawaje tukio hili la kuwapongeza mapadri
linaadhimishwa kwa mwaka “C” wa Kanisa ambao ulikuwa ni Mwaka wa Imani, na
tukio la kwanza la kihistoria kwa Parokia ya Singida; hafla hii imekuwa chachu
kwa Parokia nyingine jimboni hapa katika kuadimisha siku hii kama ilivyoazimiwa
MWISHO.
No comments:
Post a Comment