Na Evarista Lucas
Singida
Jan.24,2014
Afisa mifugo na mkaguzi wa nyama katika machinjio ya
Mitunduruni manispaa ya Singida,Edwin Shangwel Mtae,amepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi
mjini hapa;kwa tuhuma ya kupokea rushwa ya nyama ya ng'ombe kilo 12 na nusu.
Mwendesha mashitaka
na mwanasheria wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana
na Rushwa mkoa wa Singida; Bwana Dominic Maganga, mbele ya hakimu Joyce Minde
amedai kuwa ; mnamo Jeptemba 28 mwaka 2013,mtuhumiwa aliomba na kupokea rushwa
ya nyama ya ng'ombe,yenye uzito wa kilo 12 na nusu na yenye thamani ya shilingi 62,500 za kitanzania.
Amesema kuwa; kitendo alichokifanya mtuhumiwa ni kinyume
na kifungu cha 15 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa no.11/2007.
Maganga ameendelea kusema kuwa , kwa mujibu wa taarifa
walizozipokea ofisini kwao ni kwamba ; mtuhumiwa Mtae alikuwa amejenga tabia
sugu ya kuomba rushwa ya nyama za mifugo hususani maini,figo na moyo toka kwa
wafanyabishara wa nyama; ambapo mfanyabiashara asiye kubalina na ombi hilo la
rushwa ya nyama,alikuwa hawapi kibali
cha kuuza nyama ya mifugo.
Sanjari na hayo Maganga amesema; mnamo Septemba 28
mwaka 2013 majira ya asubuhi,mtuhumiwa aliwekewa mtego wa rushwa na kukamatwa
na maafisa wa TAKUKURU wa mkoa wa Singida,akiwa amepokea rushwa ya nyama kiasi
cha kilo 12 na nusu.
Kwa upande mwingine;mtuhumiwa Mtae amekanusha
kutenda makosa hayo,na kesi yake inatarajiwa kutajwa tena februari sita mwaka
huu; ambapo amefanikiwa kutekeleza masharti ya dhamana ambayo ni kuwa na
wadhamini wawili wa ahadi ya shilingi laki tano kila mmoja.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment