Na Evarista Lucas
Jan 17,2014
Singida
Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko
Kone amewaagiza madiwani wa halmashauri ya wilaya ya ikungi
manispaa ya Singida;kuwachukulia hatua kali za kisheria maafisa
maliasili,watakaobainika wanasaidia kuendeleza biashara ya mkaa.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa
upandaji miti kimkoa uliofanyika kwenye kijiji cha Nkuninkana kata ya Puma
wilaya ya Ikungi mapema jana; Kone amesema pamoja na kupigwa
marufuku kwa biashara ya mkaa mkoani humu,biashara hiyo inayotishia mkoa
kugeuka kuwa jangwa,bado inaendelea kushamiri hasa katika wilaya ya Ikungi na
Manyoni.
Amesema ; katika vijiji vya Mkiwa na
Issuna biashara ya mkaa inafanyika kwa kiwango cha kutisha na maafisa misitu wa
ngazi mbalimbali wanaangalia bila kuchukua hatua zo zote za kukomesha biashara
hii.
Aidha ; Kone amesema ili mapambano
dhidi ya biashara ya mkaa yaweze kufanikiwa,ni kuwaondoa maafisa maliasili
wanaosaidia kuendelea kwa biashara hiyo na kuweka wengine wenye moyo wa
kukomesha biashara ya mkaa.
Sanjari na hayo; Kone amewataka
wanakikundi cha nyumba ya nyuki cha kijiji cha Nkuninkana,kuhakikisha wanapanda
miti mingi ya maua kwa ajili ya chakula cha nyuki waliopo kwenye shamba lao.
Akisisitiza hilo Kone
amewaambia kuwa;bwawa la maji linatakiwa kuwa na maji ya kutiosha kipindi
chote. Pia kuwatahadharisha kuwa bila uwepo wa maji na maua ya kutosha
nyuki ni lazima watahama.
Mbali na hayo kikundi hicho
kinachojishughulisha na ufugaji nyuki wakubwa chenye miziga mia moja na ishirini
na mitatu na miziga mitatu ya nyuki wadogo;kimezawadiwa shilingi
laki tatu za kitanzania na mkuu wa mkoa wa Singida, shilingi laki tatu
mkuu wa wilaya ya Ikungi ,Manju Msambya amekichangia shilingi laki mbili.
No comments:
Post a Comment