Na, Doris Meghji Ijumaa Januari 03, 2014
Singida
Diwani wa kata ya Utemini Mh. Bartazary Kimario akifafanua hoja ya maombi maalum ya fedha za halmashuri hiyo toka serikali kuu.(Picha na Doris Meghji) |
Halmashauri ya manispaa ya Singida
imepitisha leo makisio ya mapato na matumizi shiling Bilion
31,756,044,114/= ya bajeti ya Manispaa hiyo kwa kipindi cha mwaka wa fedha
2014/2015 mkoani Singida
Diwani wa viti maalum ,Margaret Malecela na Yagi Kiaratu katika kikao cha baraza la madiwani manispaa ya singida (Picha na Doris Meghji) |
Akifunga
leo baraza maalum la bajeti la
madiniwa wa manispaa ya Singida mara baada ya kuridhia na kuungwa mkono na madiwani makisio ya bajeti ya Manispaa ya
Singida Mstahiki Meya wa Shekhe Salum Mahame ambaye ni Diwani wa kata ya
Majengo katika ukumbi wa mikutano wa manispaa ya Singida
Mstahiki Meya Salum Mahame na naibu Meya Hassan Mkata katika kikao cha baraza la madiwani Manispaa ya singida wakiwasililiza wajumbe(P |
Mstahiki Meya huyo amemtaka mkurugenzi
na wataalam wake kuhakikisha wanakusanya mapato ya kutosha ili kuweza kufikia
lengo ambayo manispaa imejiwekea katika kipindi hicho cha bajeti
Diwani Gwae Mbua Diwani wa kata ya Mtamaa,Lea Solomoni diwani viti maalum,na diwani wa kata ya mandewa manispaa ya singida |
Katika kikao cha balaza hii leo mstahiki
Meya amesema “safari sio nzuri kwako mkurugenzi na wataalam wako wote, muda
umekwisha,kwanini malengo hayafikiwi? Kwa kipindi cha 2013/2014 hadi novemba
2013 manispaa haijafikia malengo ya ukusanyaji mapato ya ndani. Utafika lini? Alihoji
mstahiki Meya
baadhi ya wataalam na waandishi wa habari katika kikao cha baraza la madiwani manispaa ya Singida(picha na Doris Meghji) |
Aidha ameongelea suala la mipango miji na
ujenzi kuwa ni moja ya eneo lenye migogoro mingi na kuwa tishio la kuwepo
kutoipenda halmashuri ya Manispaa ya Singida
Kwa upande wake mkrugenzi wa manispaa ya
Singida Joseph Mchina ameahidi kuyatekeleza yale yote yaliopendekezwa na madiwani
wa manispaa hiyo katika kikao cha chama kwa kuzingatia vipaumbele walivyojiwekea
Mstahiki meya akifunga kikao hicho cha baraza maalum la madiwani cha kupitisha bajeti(picha na Doris Meghji) |
Kwa mujibu wa Mchina amelieleza baraza
hilo la madiwani kuwa katika kipindi cha mwaka 2013/2014 mapato ya halmashuri hiyo
yameongeza kutoka kukusanya billion 1.9
hadi kufikia billion 3 ikiwa ni ongezeko kubwa ukilinganisha na kipindi
kilichopita.
Mkurugenzi wa manispaa ya Singida Ndugu Joseph Mchina akifafanua jambo kwenye kikao hicho cha madiwani (picha na Doris Meghji) |
Baadhi ya mapendekezo ya vyanzo vya mapato
ya ndani yaliyopendekezwa na waheshimiwa madiwani hao ni pamoja ongezeko la
ushuru wa vizimba vya kuuzia mbao (timber Mart) ambayo ilikuwa ni shilingi
30,000/= kwa mwaka
Sara Alute,Hadija Simba madiwani wa viti maalum wa manispaa ya singida na diwani kata ya mandewa wakipitia pitia taarifa ya bajeti ya manispaa hiyo( Picha na Doris Meghji) |
Hata hivyo jumla ya Tsh 3,500,000,000/=
zitawasilishwa na halmashuri hiyo ikiwa ni maombi maalum ya fedha toka serikali
kuu kwa lengo la ujenzi wa jengo la manispaa ambapo Tsh 2,700,000,000/ =
zitatumika, ununuzi wa gari na vifaa vya kuzolea taka ngumu na maji ni Tsh 300,000,000/=,
Tsh 200,000,000/= kwa ajili ya ujenzi wa madaraja na Tsh 300,000,000/= ni
ukamilishaji wa nyumba za walimu na madarasa ya shule za msingi
No comments:
Post a Comment