Na. Doris Meghji Jumatano Januari
15,2014
Singida
Mtoto wa umri wa mwaka moja na mwezi
mmoja ameibiwa jana na mwanamke mmoja asiyefahamika katika mtaa wa Ginery kata
ya Mandewa manispaa ya Singida
Kamanda wa polisi Mkoa wa Singida SACP Geofrey Kamwela akisoma taarifa ya jeshi hilo kwa vyombo vya habari leo ofisini kwake (Picha na Doris Meghji) |
Akitoa taarifa hiyo ya tukio kwa waandishi
wa habari leo kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida SACP Geofrey Kamwela
amesema tukio hilo limetokea jana ambapo
mtoto Meristiana Samweli mwenye umri wa mwaka mmoja na mwezi mmoja aliibiwa na
mwanamke asiyefahamika
Amesama taarifa ya kuibiwa kwa mtoto
huyo kulikuja mara baada ya mama wa mtoto huyo kubaini kuwa ameibiwa na kutoa
taarifa kwa wasamaria wema na kufika kituo cha polisi.
Kwa mujibu wa kamanda Kamwela amesema siku
mmoja kabla ya tukio mama wa mtoto huyo Fatuma Jumanne (26) mkazi wa Misuna
akiwa na mwanawe nyumbani kwake alitokea mwanamke huyo akidai anatafuta
msichana wa kazi hivyo hivyo kujenga urafiki na mama wa mtoto na kisha kuondoka
siku hiyo
siku ya tukio mwanamke huyo alirudi tena
na baada ya mazungunzo ya muda mrefu alimuomba mama na mtoto amsindikize huko eneo laa Ginery kwenda kuangalia nyumbani kwake kwa kuwa mama mwenye mtoto alikuwa na
wataoto wawaili mkubwa na mdogo yule mwanamke aliomba kumbeba mtoto mdogo,
walipofika
eneo la Ginery aliwapeleka kwenye mgahawa na kununua chai pamoja huku yeye akiwa na
mtoto mkubwa akampeleka kwenye duka moja na kumnunulia soda na hapo akamwambia wamsubiri akachukue ufunguo katika duka lililopo karibu na kuondoka na mtoto akiwa amembeba
mtoto huyo. Baaba ya kusubiri kwa muda mrefu wanamke huyo hakurudi hivyo kutokomea na mtoto
huyo kusikojulikana
Kamanda wa Jeshi La Polisi Mkoa wa Sindia SACP Geofrey Kamwela akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (Picha na Doris Meghji) |
Hata hivyo jeshi la Polisi mkoani Singida linawaomba wananchi wa mkoa wa singida kutoa taarifa kwa serikali ya
mtaa, kijiji, na kituo cha polisi chochote wakimuona mtu yoyote mwenye mtoto
mdogo mwenye umri wa mwaka mmoja na mwezi mmoja atakayeonyesha dalili za mtoto
kutokuwa wake
Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi
mkali wa tukio hilo
Mwisho
No comments:
Post a Comment