Na Evarista Lucas
Singida
Jan.02, 2014
Imeripotiwa
kuwa watu wawili wamepoteza maisha katika matukio mawili tofauti mkoani
Singida; ambapo katika tukio la kwanza Mwanahamisi Mwangu mwenye umri wa miaka
72 amepoteza maisha baada ya kupigwa
mateke na ngumi na Salehe Mohammed mume wake wa ndoa Salehe Mohammed mwenye
umri wa miaka 75.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mkoani
hapa; Kamanda wa polisi mkoa wa Singida bwana Geofrey Kamwela amesema; marehemu Mwanahamisi
alipoteza maisha kutokana na kupigwa mateke na ngumi na mume wake hali iliyopelekea kifo ni chake.
Kamwela amesema tukio hilo lilowahusisha
wanandoa hao ambao ni wakazi wa kijiji cha Mwasutianga kata ya Irisya wilaya ya
Ikungi mkoani hapa; limetokea desemba 30 mwaka jana majira ya saa saba mchana
huko katika kijiji cha Mwasutianga.
Kamwela amesema siku ya tukio,mzee Salehe
alikuwa akilima shambani kwake na mke wake mkubwa Mwanahamisi na mke mdogo
Fatuma Ramadhani (55).wakati wandoa hao wakiendelea kulima,ghafla kulizuka
ugomvi baina ya wake wa mzee Salehe wakigombea ndoo ya maji ambayo inadaiwa
ilikuwa mali ya mke mdogo Fatuma.
Kamwela amesema mtuhumiwa mzee Salehe katika
ugomvi huo,alikuwa upande wa mke mdogo ambapo alianza kumpiga mateke na ngumi
katika sehemu za mwili wa mke mkubwa Mwanahamisi na kusababisha kifo chake papo
hapo
Katika tukio jingine Kamwela amesema Shauri
Samwel (22) mkazi wa kijiji cha Tyeme tarafa ya Shelui wilaya ya
Iramba,amefariki dunia baada ya kunywa vidonge vya kuhifadhia nafaka
vinavyodhaniwa kuwa na sumu kali.
Amesema tukio hilo limetokea desemba 31 mwaka
jana saa 12 jioni huko katika zahanati ya kijiji cha Tyeme wakati Shauri
alikuwa akiendelea kupatiwa matibabu.
Kamwela amesema chanzo cha kunywa vidonge hivyo
vya sumu,ni hofu aliyokuwa nayo Sahauri kutokana na kumpa mimba binamu yake.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment