Monday, January 20, 2014
Breaking News:AJALI MBAYA SINGIDA
Na Doris Meghji
Jumatatu 20, Januari 2014
Maiti wakiendelea kunasuliwa toka katika mabaki ya gari walilokuwa wakisafiria toka Itigi kuelekea Singida mjini
Polisi wakibeba miili ya maiti waliokuwa wakisafiri katika gari aina ya Noah
Ajali mbaya iliyohusisha gari aina ya Noah na gari kubwa imetokea leo Singida katika kijiji cha Isuna. Katika ajali hiyo kati ya abiria 14 abiria 13 waliokuwa wakisafiri na gari la Noah kutokea katika mji wa Itigi kwenda Singida mjini wamefariki papo hapo baada ya Roli hilo lilokuwa limebeba samaki likisafiri kuelekea Dar-es Salaam kugongana uso kwa uso kwa kile kilichoelezwa dereva wa Roli hilo kuendesha upande usiokuwa wake. Polisi mjini hapa wanaendelea kumtafuta dereva wa Roli hilo baada ya kusababisha ajali na kukimbia kukimbia.
__________________________________MWISHO________________________________
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment