Na Evarista Lucas
Singida
Januari 01,2014
Imeelezwa kuwa
kwa kipindi cha kati ya mwezi ya Januari na Desemba mwaka jana; Taasisi ya
kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoani Singida, imepokea taarifa mia
moja na mbili za malalamiko dhidi ya vitendo vya kuomba na kupokea rushwa.
Akitoa taarifa kwa vyomba vya habari mapema juzi juu
ya utekelezaji wa majukumu yake kwa kipindi cha kuanzia januari hadi desemba
mwaka jana; mkuu wa TAKUKURU mkoani hapa
Bwana Joshua Msuya amesema kuwa kati ya taarifa hizo, themanini na saba ziko
kwenye uchunguzi wa hatua mbali mbali, kumi na tatu zilitolewa ushauri kwa
walalamikaji na mbili zimehamishiwa
katika idara nyingine.
Sanjari na hayo
Msuya amesema kuwa taarifa hizo za mwaka jana, ni ongezeko la asilimia 11.7
ikilinganisha na taarifa 94 za mwaka juzi na kuongeza kuwa katika taarifa hizo,
watuhumiwa wa jinsi ya kike ni kumi na saba na taarifa themanini na watano watuhumiwa wake ni wa jinsi ya kiume. Akifafanu
zaidi, mkuu huyo,alisema taarifa hizo za mwaka jana, ni ongezeko la asilimia
11.7 ikilinganisha na taarifa 94 za mwaka juzi.
Msuya amesema
ongezeko la taarifa linatokana na jitihada za kutoa semina na elimu kwa
wananchi na makundi mengine katika jamii ambazo zilifanywa na TAKUKURU mkoa zikiwa
na lengo la kuwajengea ujasiri walengwa juu ya kuvifichua na kuvipinga vitendo vya rushwa.
Katika hatua
nyingine, Msuya alitaja baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo ambazo ni
jukumu la kupambana na rushwa kuchukuliwa kuwa ni la TAKUKURU peke yake na kukosekana
kwa uzalendo miongoni mwa baadhi ya wananchi, kiasi kwamba mtu akiona vitendo
vya rushwa vinafanyika, anaona sio jukumu lake kuvikemea.
TAKUKURU mkoani
hapa imeanzisha Klabu za kupinga na kupambana na rushwa kwa ngazi za shule za
sekondari na vyuo kwa lengo la kuwajengea uelewa na mazingira ya kuichukia
rushwa na kuripoti vitendo vya rushwa.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment