Na,Doris
Meghji Jumanne Januari 28,2014
Singida
Zao la mtama mkoani Singida linatarajiwa
kuwa mkombozi kwa wananchi na wakulima wa mkoa huo kiuchumi.
Mkuu wa wilaya ya Singida Mwl. Queen Mulozi akiwa ofisini kwake jana(Picha na Doris Meghji) |
amesema “fursa imekuja ya zao la mtama
kuwa zao la biashara, wakulima wakaze buti kuhakikisha tunajikita kwenye kilimo
cha kuleta tija na kuondokana na umaskini” alisema mkuu huyo wa wilaya
aidha katika maandalizi ya kutekeleza
mpango huo wa ulimaji wa zao la mtama wiliya ya singida na mkoa kwa ujumla
umepanga kuanzisha mashamba ya bega kwa bega badala ya kuwa na shamba mmoja la
mtama liwe hapa na lingine kule kwa lengo la kuwa karibu.
Mwl.Queen Mulozi Mkuu wa wilaya ya Singida (picha na Doris MeghjI) |
Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya ya Singida
amesema katika bajeti ya 2014/2015 kila halmashauri imeagizwa kununua mashine tano
za kupura mtama likiwa ni agizo la mkuu wa mkoa wa Singida Dr. Parseko Kone ikiwa
ni moja ya maandalizi ya kulima zao hilo kibiashara katika kusaidia mkulima
kuzuia upotevu wa zao hilo nyakati za uvunaji na uhifadhi wa zao hilo
kwa mujibu wa mkuu huyo wa wilaya
amesema baadhi ya mabenki ya CRDB na NMB mkoani singida yako tayari kukopesha
wakulima fedha kwa ajili ya kununua mashine hizo hivyo kilimo hicho cha
biashara cha zao hilo la mtama kinatarajiwa kuanza rasmi mwaka 2015.
Mkuu wa wilaya ya Singida Queen Mulozi akisisitiza jambo juu ya fursa ya soko la zao la mtama katika mkoa wa singida (picha na Doris Meghji) |
Mwl Mulozi amewapongeza wananachi wa
wilaya yake kwa jitihada walizozionyesha mwaka huu katika msimu wa kilimo
amesema “hali inaridhisha ya msimu huu wa kilimo nimepita tarehe tisa mwezi
januari na tarehe 12 mwezi januari nimejiridhisha kama mvua zitaendelea vizuri
kunyesha hatutakuwa na shida ya upungufu wa chakula, maeneo ya kama Merya,Msange,Ukhandi,Makuro
Ikhanoda hali ya kilomo cha mtama kiko vizuri.alisema mkuu huyo.
vitunguu ni mmoja ya zao la biashara liloanishwa katika kitabu cha muongozi cha kilimo na mifugo mkoa wa singida (picha na Doris Meghji) |
Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi na
wakulima wa wilaya yake kuendelea kulima mazao ya biashara na chakula
yaliyoanishwa katika kitabu cha muongozo wa kilimo na mifugo cha mkoa wa singida
kulingana na hali ya hewa ya mkoa huo kwa kulima mazao ya alizeti,vitunguu,pamba,uwele,mtama,mhogo,viazivitamu
na zao la asali kupitia ufugaji nyuki kwa kutunza misitu katika maeneo yao.
mwisho
No comments:
Post a Comment