Na, Doris Meghji Jumatano 01 Januari 2014
Singida
Waumini wa Jimbo Katoliki la Singida
wameombwa kuendelea kuomba amani duniani hasa nchi ya Tanzania ili iendelee
kuwa kisiwa cha amani kwa kuwataka wanakanisia kutokuwa chanzo cha uvunjivu wa
amani.
Hayo yamesema katika misa takatifu ya
kuukaribisha mwaka 2014 iliyoadhinishwa Padre
Paterini Mangi na Mwenzake kuanzia saa 5 usiki disemba 31 2013 katika Kanisa la
Moyo Mtakatifu wa Yesu Jimbo la Singida
Padre huyo amewaasa wanakanisa wa kanisa
hilo kuwataka kuwa chanzo cha amani kuachana na mambo ya kulipiza visasi “
visasi sio suluhisho la kupata amani tusichoke kuomba amani kwa nchi yetu ili
watu wa Tanzania wafurahiye matunda na rasilimali zilizopo katika nchi yao”alisisitiza
Padre huyo
Aidha amewataka waumini kujiwekea
malengo ya kiroho zaidi hasa mwaka 2014 ambao Baba Mtakatifu ameutanganza kuwa
ni mwaka wa kifamilia kwa waunini kujiepusha na dhambi hivyo kwa kujiweka
malengo ya kiroho na kimwili ili wawe karibu na mwenyezi Mungu.
Waumini hao wametakiwa kumshukuru
Mwenyezi Mungu kwa kuwalinda na kuwafadhili kwa wao kufikia siku hiyo ya leo
kwa kuomba Baraka kwa Mungu atujalie uzima.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment