Vifo
Na Evarista Lucas
Jan 17,2014
Imeripotiwa kuwa; watu watatu
wamepoteza maisha mkoani Singida katika matukio tofauti ya kogongwa
na magari katika nyakati tofauti tofauti mwanzoni mwa mwaka huu wa 2014..
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari
ofisini kwake mapema leo; Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida bwana
Geofrey Kamwela,amesema katika tukio la kwanza ambalo limetokea januari
14 mwaka huu saa 11.00 jioni huko Itigi wilayani Manyoni mkazi wa Itigi
wilayani hapo aliyefahamika kwa jina la Katendere Nyiga (60), amefariki dunia
baada ya kugongwa na gari lenye namba T.275 APE mali ya Nurdini Mshana.
Kamwela amesema katika
tukio jingine mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Ulyampiti
wilayani Ikungi Amri Labia (12) ,amefariki dunia baada ya kugongwa na gari.
Amesema; tukio hilo limetokea
januari 14 mwaka huu saa 11.30 jioni huko katika kijiji cha Ulyampiti na kusema
kuwa mwanafunzi huyo amegongwa na gari yenye namba T.BBB aina ya Toyota land
cruiser mali ya kanisa katoliki jimbo la Singida lilokuwa likiendeshwa na
Padre wa Manyoni mjin bwana John Vustan (48) i .
Aidha katika tukio jingine,Kamwela
amesema mkazi wa Kibaoni kata ya Kindai tarafa ya Mungumaji manispaa ya
Singida,bi Pili Ally (30) amefariki dunia januari 14 mwaka huu saa mbili usiku
baada ya kugongwa na gari lenye namba T.529 BLL.
Amesema;mtembea kwa miguu huyo
amegongwa na gari la maji machafu wakati akivuka barabara kuu ya
Singida-Dodoma,lakini ghafla alirudi tena upande alikotoka na hatimaye
kugongwa.
No comments:
Post a Comment